Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 19. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Yesu alitumia usemi gani mara nyingi kukazia wasikilizaji wake usahihi wa maelezo yake? (Mathayo 5:18)
2. Ni nani ambaye ilisemwa juu yake hivi: “Aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu”? (1 Mambo ya Nyakati 12:8-14)
3. Ni nani ambaye jina lake huhusianishwa na wapiganaji mashujaa wa Daudi waitwao Yoabu, Abishai, na Asaheli? (2 Samweli 2:18)
4. Ijapokuwa huenda mtu akawa kitu cha kuchukiwa kwa sababu ya jina la Yesu, yeye alisema lazima mtu afanye nini ili aokoke? (Marko 13:13)
5. Hamani alikuwa na wana wangapi, ambao waliuawa wote kwa sababu ya uhasama wake kwa Wayahudi? (Esta 9:10)
6. Ni aina gani ya kiumbe wa kiroho aliyegusa midomo ya Isaya kwa kaa la moto ili Isaya atimize mgawo wake wa unabii? (Isaya 6:6)
7. Ni nani aliyekuwa “mtu mwenye kusimamia” wa Herode, ambaye mke wake Yoana, alimhudumia Yesu? (Luka 8:3)
8. Paulo aliwatia moyo wanaume katika kutaniko wafikie cheo gani chenye daraka? (1 Timotheo 3:1)
9. Ni yapi majina ya mito minne iliyoenea kutoka ‘mto utokao Edeni’? (Mwanzo 2:10-14)
10. Paulo alitaja kwamba chachu kidogo ilikuwa na uwezo wa kufanya nini? (Wagalatia 5:9)
11. Majina ya wana watatu wa Noa yalikuwa nani, ambao kutoka kwao “nchi yote ikaenea watu”? (Mwanzo 9:18, 19)
12. Ni nani aliyekuwa baba ya nabii Samweli? (1 Samweli 1:19, 20)
13. Ni karibu na jiji lipi muhimu lenye kuelekea Bonde la Yezreeli ambapo vita vingi vya kukata maneno vilipiganwa? (Waamuzi 5:19)
14. Wakiokolewa kwa sababu ya ujanja wao, Wagibeoni waligawiwa kazi gani? (Yoshua 9:27)
15. Ni jina gani walilopewa wale wanafunzi 12 ambao Yesu aliwateua binafsi? (Mathayo 10:2)
16. Ni vyeo gani vya Yesu pekee ambavyo aliwaambia wanafunzi wake hawapaswi kuitwa? (Mathayo 23:8, 10)
17. Paulo aliandika kitabu cha Waebrania katika nchi gani? (Waebrania 13:24)
18. Ni usemi gani ambao Yobu alitumia kueleza kwamba alikuwa amenusurika kifo? (Ayubu 19:20)
19. Katika nyakati za kale, ni wapi ambapo nafaka ilitenganishwa na mabua na makapi? (Ruthu 3:3)
20. Kwa sababu gani ndugu za Yosefu walimchukia? (Mwanzo 37:3-11)
Majibu ya Maswali
1. “Kwa kweli nawaambia nyinyi”
2. Wanaume chapuchapu na mashujaa wa kabila la Gadi waliojiunga na Daudi nyikani alipokuwa angali kwenye vizuizi kwa sababu ya Mfalme Sauli
3. Mama yao, Zeruia
4. Avumilie mpaka mwisho
5. Kumi
6. Serafi
7. Kuza
8. “Cheo cha mwangalizi”
9. Pishoni, Gihoni, Hidekeli, na Frati
10. Huchachusha donge lote
11. Shemu, Hamu, na Yafethi
12. Elkana
13. Megido
14. Walikuwa ‘wapasuaji wa kuni na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote na madhabahu ya Yehova’
15. Mitume
16. Rabi na Kiongozi
17. Italia
18. “Nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu”
19. Kwenye sakafu ya kupuria
20. Kwa sababu baba yake alimpenda sana na kwa sababu ya ndoto alizokuwa nazo