Eneo la Makaburi Lisilo la Kawaida
Eneo la Makaburi Lisilo la Kawaida
NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA EKUADO
KATIKA mji wa Ibarra, kaskazini ya jiji kuu la Ekuado, Quito, kuna eneo la makaburi lisilo la kawaida—el cementerio de los pobres (Makaburi ya Watu Maskini). Ni nini kinachofanya eneo hilo lisiwe la kawaida? Michoro iliyo kwenye ukuta wa nje ni picha kutoka kwa vichapo vya Watch Tower Society zilizonakiliwa kikamili na kufanywa kubwa! * Kuna mchoro wa mtume Yohana katikati, ulionakiliwa kutoka ukurasa wa 7 wa kitabu cha Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Juu ya Yohana, kuna andiko hili katika Kihispania: “Ufalme wa Mungu wamaanisha uadilifu na amani na shangwe. Waroma 14:17.” Kati ya hizo picha mbili kuna maneno ya Mathayo 11:28: “Njoni kwangu, nyingi nyote mnaomenyeka na kulemezwa mizigo, nami hakika nitawaburudisha nyinyi,” yaliyofasiliwa kutoka kwa Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Bila shaka ukuta huu wa eneo hilo la makaburi unaelekeza watu kwa Neno la Mungu.
[Maelezo ya Chini]
^ fu. 3 Ili kutekeleza matakwa ya kisheria, ni lazima idhini itolewe kabla ya kunakili makala au kuchora picha kutoka kwenye vichapo vya Watch Tower, na yapasa kuonyeshwa kwamba zimetoka kwa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania.