Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kito cha Mwitu

Kito cha Mwitu

Kito cha Mwitu

KATIKA MAJANGWA makavu ya Afrika, ambako mvua huwa nadra, humea kito—waridi la jangwani. Mmea huu wenye umbo la kuvutia, majani yenye mikunjo-mikunjo, hukua polepole na yasemekana kwamba huishi kwa mamia ya miaka. Shina pana la mti huo na mizizi yake huhifadhi maji, likiuwezesha kusitawi katika mazingira makavu, yasiyokalika.

Mizizi na mbegu zenye utomvu ulio na maziwa ya mmea huu wenye maji mengi, ina sumu hatari. Utomvu wa mbegu zake hutumika kutia sumu ncha za mishale, na wavuvi wenyeji hurusha matawi yake ndani ya maji kutia samaki bumbuazi ili wawanase kwa urahisi. Kwa kuongezea, wachungaji hutumia sehemu ya mmea huo kutayarishia sumu inayoua kupe na chawa kwa ngamia na ng’ombe zao. Kwa kushangaza, licha ya sumu ya mti huo, wanyama wa pori hula majani yake bila kudhuriwa.

Lakini waridi lenye sumu la jangwani laweza kuitwaje kito? Likiwa na vichala vya machanuo yenye kuvutia, waridi la jangwani ni lenye kustaajabisha, likiwa na rangi mbalimbali nyangavu kuanzia nyekundu-nyeupe hadi nyekundu kabisa. Nchi inapokuwa kavu bila rangi ya kupendeza, kito hiki cha jangwani huwa na maua mengi yanayong’aa yanapoangazwa na jua.

Urembo huo wenye kushangaza jangwani ni kikumbusho tu cha wakati ambapo “nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua.” (Isaya 35:1) Ahadi hiyo yenye kupendeza kwa kweli itatimizwa kihalisi chini ya utawala unaokuja wa Ufalme wa Mungu. Wakati huo dunia yote ‘itashangilia,’ si ikiwa paradiso ya kupendeza tu bali pia mahali pa amani kwa wanadamu wote.—Zaburi 37:11, 29; Isaya 35:6, 7.

[Picha katika ukurasa wa 31]

© Mary Ann McDonald