Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Upendo Unaposhindwa Kuona

Upendo Unaposhindwa Kuona

Upendo Unaposhindwa Kuona

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA HISPANIA

EBU wazia ukitafuta bibi-arusi huku ukiwa na tatizo la kutoona mbali na ikiwa wanawali wanaofaa wanatoka nje usiku tu. Hiyo ndiyo hali ya nondo-maliki wa kiume. Lakini mdudu huyu mwenye madaha ana sifa fulani zinazopunguza uzito wa tatizo hilo kubwa.

Katika miezi ya kiangazi, nondo anayetafuta mchumba huishi kwa siku kadhaa akiwa kiwavi mnene anayebugia chakula chote anachoweza kupata. Hivyo, majira ya masika yafikapo, yeye huibuka kutoka kwenye pupa, na nondo huyo mwenye kung’aa huhifadhi mlo wa kutumiwa muda mfupi wa maisha yake.

Akiwa na chakula cha kutosha, nondo-maliki aweza kukazia kazi ya kutafuta mwenzi. Hata hivyo, kama hangelikuwa na kifaa fulani mwilini mwake, ingelikuwa vigumu sana kwake kupata nondo wa kike katika mbalamwezi.

Kichwa kidogo sana cha nondo huwa na vipapasio viwili vinavyoshabihi kangaga. Sehemu hizi ndogo mno zaweza kuwa vifaa tata zaidi ulimwenguni vya kunusia harufu. Zaidi ya hayo, vimefanyizwa kwa njia bora sana kuweza kunusa hata chembe ndogo sana za kemikali za viumbe, au “manukato,” yanayotokezwa kiasili na nondo wa kike.

Ijapokuwa nondo wa kike waweza kuwa wachache sana, kemikali yenye harufu kali watoayo huenea mbali. Vipapasio vya nondo wa kiume vina nguvu sana kiasi cha kuweza kumtambua nondo wa kike aliye umbali wa kilometa 11 hivi. Kwa hiyo, vizuizi vyote huepukwa, na hatimaye nondo wa kiume hukutana na wa kike. Upendo waweza kushindwa kuona kwa habari ya wadudu—angalau katika kisa hiki.

Uumbaji wa Mungu una mambo mengi madogo ya kuvutia sana na ubuni wa ajabu! Mtunga-zaburi aliandika hivi: “Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia.”— Zaburi 104:24.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 10]

© A. R. Pittaway