“Vitabu Vingi vya Mafundisho vya Chuo Kikuu Si Sahihi Jinsi Hiyo”
“Vitabu Vingi vya Mafundisho vya Chuo Kikuu Si Sahihi Jinsi Hiyo”
Hiyo ilikuwa sehemu ya uchunguzi wa mtu mmoja kuhusu kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali? Mmoja wa Mashahidi wa Yehova huko Sydney, Australia, alimwangushia kitabu hicho. Jioni hiyo Shahidi alikuta ujumbe ufuatao kwenye mashine yake ya kujibia simu.
“Nilizungumza nawe leo asubuhi. Nimesoma nusu ya kitabu ulichoniachia asubuhi—“Je, Kuna Muumba Anayekujali?” Nimepiga simu kwa sababu nimeshtuka kuona jinsi kitabu hiki kilivyo cha kisasa na sahihi kuhusu mwanzo wa ulimwengu. Kina ujuzi uleule kama wa kitabu nilichokuonyesha . . .
“Kitabu chenu ni sahihi sana na cha kisasa! Vitabu vingi vya mafundisho vya chuo kikuu si sahihi jinsi hiyo. Chataja zile kani nne za msingi—nguvu ya uvutano, sumaku-umeme, kani ya nyuklia yenye nguvu, na kani dhaifu ya nyuklia. Huo ni uvumbuzi wa karibuni zaidi na wa wakati huu. Nitaongea nawe juma lijalo. Kwaheri.”
Wewe pia waweza kupata nakala ya kitabu hiki chenye kurasa 192 kilicho na jalada la karatasi kwa kujaza na kutuma kuponi iliyopo hapa ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.
□ Nitumieni nakala ya kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali?
□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia nyumbani bila malipo.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]
J. Hester and P. Scowen (AZ State Univ.), NASA