Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mfungwa Aweza Kujifunza Nini Kutokana na Ndege?

Mfungwa Aweza Kujifunza Nini Kutokana na Ndege?

Mfungwa Aweza Kujifunza Nini Kutokana na Ndege?

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA AFRIKA KUSINI

KULINGANA na gazeti Sunday Tribune la Durban, Afrika Kusini, ndege wanashiriki fungu fulani la kulainisha mioyo ya wafungwa katika Gereza la Pollsmoor. Sasa kuna wafungwa 14 wanaoshiriki katika programu inayohusisha kutunza cockatiel na kasuku-mapenzi ndani ya seli zao.

Programu hiyo hufanyaje kazi? Kila mfungwa anayeshiriki ana kiangulio cha muda ndani ya seli yake. Kifaranga kilichoanguliwa hutunzwa na mfungwa, ambaye hulisha kiumbe huyo asiyejiweza kila baada ya muda wa saa moja au mbili usiku na mchana kwa muda wa majuma matano hivi. Kisha ndege huyo huwekwa ndani ya kizimba, ambacho pia huwekwa ndani ya seli. Ndege akuapo, huuzwa kwa umma. Wafungwa fulani huwa na uhusiano wa karibu sana na ndege wao hivi kwamba hulia wanapolazimika kuachana nao.

Hata wahalifu fulani walio sugu wameonekana kuwa wanana baada ya kuzungumza na kuwatunza ndege kila siku. Mfungwa mmoja alisema: “Mimi huwatiisha ndege, lakini wao pia wamenitiisha.” Mwingine asema kwamba ndege walimfunza kuwa mwenye saburi na kujidhibiti. Mwizi aliyepatikana na hatia asema kwamba kutunza ndege kulimfanya ang’amue kwamba kuwa mzazi “ni daraka zito”—daraka alilopuuza kuelekea watoto wake mwenyewe alipokuwa huru.

Kutunza ndege hao huleta manufaa nyingine kwa wafungwa. “Kwa kutumia stadi walizojifunza hapa, wanaweza kupata kazi kwa wafugaji-ndege na daktari wa wanyama, wanapoachiliwa kutoka gerezani,” asema Wikus Gresse, mwanzilishi wa programu hiyo.