Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Maliki wa Ajabu

Maliki wa Ajabu

Maliki wa Ajabu

PENGWINI mkubwa kuliko wote aitwaye emperor (maliki), ana urefu wa zaidi ya meta moja na uzito wake unaweza kufikia kilogramu 40. Pengwini wengine wanapoelekea kaskazini ili waepuke majira ya baridi kali yenye giza ya Antaktika, emperor huelekea kusini—kwenda Antaktika! Kwa nini? Jambo la kushangaza ni ili kutaga na kuangua mayai.

Pengwini emperor wa kike anapotaga yai lake, emperor wa kiume analichukua mara moja lisikae kwenye barafu na kuliweka juu ya nyayo zake. Ndipo analiingiza chini ya kifuko chake cha kuatamia—hicho ni mkunjo wa ngozi katika sehemu ya chini ya tumbo lake. Kisha emperor wa kike anaelekea bahari isiyofunikwa kwa barafu panapopatikana chakula. Kwa siku 65, katika hali ya hewa mbaya isiyo ya kifani, emperor wa kiume huatamia mayai akipata lishe kutokana na mafuta yake ya mwilini. Ili kuhifadhi joto la mwili wanapostahimili dhoruba kali za theluji zenye mwendo wa kasi wa kilometa 200 kwa saa, ndege hao werevu husongamana katika makundi makubwa, huku kila mmoja akishika zamu yake ya kusimama katika mstari wa nje ili akinze upepo kwa mgongo wake.

Ajabu ni kwamba vifaranga wanaanguliwa wakati barabara emperor wa kike wanaporudi. Lakini awezaje kupata mwenzi wake kati ya maelfu ya ndege wanaofanana kabisa? Kwa kutumia wimbo. Wakati wa uchumba wao, wenzi hao waliimbiana, na kila mmoja akaweka wimbo wa mwenzi akilini. Huyo emperor wa kike warudipo, emperor wote, wa kike na wa kiume huimba kwa moyo wote. Wanadamu wangevurugwa kabisa na makelele hayo, lakini emperor hao huwapata wenzi wao kwa urahisi. Ndipo, baada ya kumkabidhi emperor wa kike kifaranga kilichoanguliwa karibuni, emperor wa kiume wenye njaa kali huvuka, kwa kutembea ama kwa kuteleza kwa tumbo, sehemu yenye barafu ya kilometa 72, akitafuta bahari isiyofunikwa kwa barafu ambapo chakula kitapatikana.

[Picha katika ukurasa wa 31]

By courtesy of John R. Peiniger