Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 22. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Ni nani ambaye mtume Yohana aliona “katikati ya vinara vya taa,” akimpa ujumbe wa makutaniko saba? (Ufunuo 1:13)

2. Badala ya kujiacha ‘tushindwe na lililo ovu,’ Paulo anatushauri tufanye nini? (Waroma 12:21)

3. Yesu alimaanisha nini aliposema: “Ikiwa mtu fulani aliye chini ya mamlaka akushurutisha ufanye utumishi kwa kilometa moja, nenda pamoja naye kilometa mbili”? (Mathayo 5:41)

4. Badala ya kusonga nywele na kujipamba kwa madoido ya dhahabu, Petro alishauri wake Wakristo wajirembe kwa kitu gani? (1 Petro 3:3, 4)

5. Isaya alimwitaje Abrahamu, ikionyesha kwamba alikuwa baba wa kibinadamu wa taifa la Israeli? (Isaya 51:1)

6. Kwa nini Daudi alikataa kunywa maji ambayo mashujaa watatu walimletea kutoka Bethlehemu, alipokuwa kwenye pango la Adulamu? (2 Samweli 23:15-17)

7. Bath-sheba alikuwa anafanya nini Daudi alipomwona kwa mara ya kwanza? (2 Samweli 11:2)

8. Badala ya wino, Paulo alisema kwamba mioyo ya Wakristo Wakorintho ilikuwa imeandikwa kwa kitu gani? (2 Wakorintho 3:3)

9. Yehova aliondoaje nzige wa pigo la nane, asisalie hata mmoja katika Misri? (Kutoka 10:19)

10. Kwa sababu gani Yehova alimwua Sauli? (1 Mambo ya Nyakati 10:13)

11. Paulo alibadilisha mashua katika jiji gani lenye bandari alipokuwa akielekea Roma akiwa mfungwa? (Matendo 27:5)

12. Yehova alionyeshaje hangaikio kwa wajane na watoto yatima katika Israeli la kale? (Kutoka 22:22-24; Kumbukumbu la Torati 24:17-21)

13. Shamba ambalo makuhani walinunua kwa fedha ambazo Yudasi alitupa hekaluni liliitwaje? (Mathayo 27:3-8; Matendo 1:19)

14. Kwa nini Petro alimkaripia Simoni kwa ukali kwa kumpa fedha ili awe na mamlaka ya kuwapa watu roho takatifu? (Matendo 8:20, 21)

15. Sara alikuwa na umri wa miaka mingapi alipomzaa Isaka? (Mwanzo 17:17)

16. Elimeleki na mke wake Naomi, walihamia nchi gani kwa sababu ya njaa, mahali ambapo mwana wao Maloni alimwoa Ruthu? (Ruthu 1:1-4)

Majibu ya Maswali

1. Yesu Kristo, ambaye Yohana alimtaja kuwa “mtu fulani kama mwana wa binadamu”

2. “Fuliza kushinda lililo ovu kwa lililo jema”

3. Alikuwa akionyesha uhitaji wa kunyenyekea kwa hiari madai yaliyo halali

4. “Vao lisilofisidika la roho ya utulivu na ya upole”

5. “Mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa”

6. Kwa sababu yaliwakilisha damu yao, ambayo walikuwa wameihatarisha ili kuyapata

7. Akioga

8. “Kwa roho ya Mungu aliye hai”

9. Upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi uliwapeleka katika Bahari ya Shamu

10. Alikosa uaminifu kumwelekea Yehova kwa kutofuata maagizo yake na kwa kumwendea mwasiliani-roho

11. Mira katika Likia

12. Aliwaandalia hali njema na riziki yao

13. Akeldama, au “Shamba la Damu”

14. Alionyesha mwelekeo mbaya kwa kujaribu kununua hiyo “zawadi ya bure ya Mungu,” na moyo wake haukuwa “mnyoofu mbele ya macho ya Mungu”

15. Alikuwa na umri wa miaka 90

16. Moabu