Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Karne ya Ishirini Toleo la Desemba 8, 1999, lilikuwa zuri sana! Nilinufaika sana, hasa na ule mfululizo “Karne ya 20—Miaka Muhimu ya Badiliko.” Lilikuwa lenye kuarifu na sahili. Lilinifanya nitamani kuwa macho zaidi kiroho katika siku hizi za mwisho.

M. V., Filipino

Utekaji-Nyara Mfululizo “Utekaji-Nyara—Sababu Ni Tisho la Tufeni Pote” (Desemba 22, 1999) ulikuwa na ujumbe mzuri kama nini! Makala hiyo ilitokea wakati ambapo ulimwengu mzima ulikuwa ukitazama kwa hamu tukio la kutekwa nyara kwa ndege ya Shirika la Ndege la India mnamo Desemba 24. Laiti wasimamizi wangesoma na kutumia madokezo yaliyotolewa katika makala yenu kuhusu kudhibiti utekaji-nyara!

A. S., India

Mtu Aliyezimia kwa Muda Mrefu Asanteni kwa simulizi la Michiko Ogawa. (“Tumaini Limenitegemeza Kuvumilia Majaribu,” Desemba 22, 1999) Mume wake alipatwa na aksidenti nilipokuwa na umri wa siku tano. Nashindwa kuwazia kwamba amekuwa bila fahamu karibu muda wote wa maisha yangu! Kwa kweli Yehova amemsaidia kulea wavulana wake wawili na kuvumilia hali hii yenye kujaribu.

L. N., Marekani

Moyo wangu uliguswa sana na makala hiyo. Mimi huishi peke yangu na hivi majuzi niligundua kwamba nina kansa. Baada ya kusoma makala hiyo, nilitaka kumkumbatia Michiko na kumshukuru kwa kuwa mwaminifu kwa Yehova licha ya majaribu. Nilipopatwa na kansa, kwanza nilitaka muujiza fulani utendeke. Lakini sasa, kama Michiko, nataka tu mapenzi ya Yehova yatendeke.

M. S., Marekani

Tiba Bila Damu Ule mfululizo “Tiba na Upasuaji Bila Damu—Uhitaji Unaoongezeka!” (Januari 8, 2000) ulifanyiwa utafiti wa hali ya juu. Ninahudhuria shule ya uuguzi na nilimpa mwanafunzi mwenzangu na pia mmoja wa walimu wangu gazeti hilo. Wakati fulani uliopita watu hao walikuwa wakiwabagua Mashahidi wa Yehova. Lakini walifurahi kupokea makala hizo pamoja na habari nyingineyo kuhusu Mashahidi wa Yehova.

R. P., Uswisi

Watoto wangu wawili walihusika katika aksidenti ya gari mwaka wa 1998. Mguu wa mwana wangu ulivunjika. Alisema tena na tena kwamba hakutaka damu! Lakini hospitali haingeweza kumfanyia upasuaji bila damu. Alihamishwa hadi hospitali nyingine, lakini wafanyakazi wa hospitali hiyo hawakutaka kumfanyia upasuaji kabla kiwango chake cha damu hakijafikia 35. (Kilikuwa kimeshuka sana hadi 8.1.) Walikuwa na mtazamo wa uzembe, kana kwamba walikuwa wakingoja tu ikiwa atakufa. Hata hivyo, walipokuwa wakitumia mbinu zisizohusisha damu—kuinua mguu wake, kutumia erythropoietin, na kadhalika—kiwango chake cha damu kiliongezeka na kufikia 35.8! Upasuaji huo ulifaulu, lakini kwa sababu ya kuchelewa kutibiwa, alipatwa na madhara makubwa ya kudumu. Laiti kila daktari, daktari-mpasuaji, na daktari-nusukaputi wangeamriwa kusoma makala hizo.

L. L., Marekani

Inafariji kujua kwamba madaktari wengi wanakubali kushirikiana na Mashahidi wa Yehova. Nitampelekea daktari wangu gazeti hili mara moja. Najua litampendeza.

U. M., Marekani

Makala hiyo ilitokea wakati tu nilipopanga kufanyiwa upasuaji. Kiwango changu cha damu kilipopungua kwa sababu ya kuvuja damu sana, nilitumia gazeti hilo kuwaeleza wafanyakazi wa hospitali na washiriki wa familia kwa nini sitakubali damu. Kwa msaada wa Yehova nimepona kabisa.

C. B., Marekani