Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 14. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Iwe ni ya mwanadamu, mnyama, au mazao, Yehova alitaka nini kitolewe kwake? (Mithali 3:9)

2. Katika sheria, Yehova alisema ni chombo kipi cha mkulima huenda kikatumiwa isivyofaa kuwa silaha? (Kutoka 21:18, NW)

3. Katika matayarisho ya kujengwa kwa hekalu, Mfalme Daudi aliwapa wageni mgawo upi? (1 Mambo ya Nyakati 22:2)

4. Wakiwa njiani kwenda Emausi, ni nani aliyesema kwamba huenda Yesu akawa mkazi-mgeni kwa sababu alionekana hajui yaliyokuwa yametukia Yerusalemu? (Luka 24:18)

5. Ni nani sikuzote huonyeshwa akiwa mwana wa pili wa Noa, ijapokuwa huenda alikuwa ndiye mwana mchanga zaidi? (Mwanzo 5:32)

6. Ni yupi kati ya makuhani wa ukoo wa Aroni aliyejulikana kuwa mnakili na mwalimu stadi wa Sheria? (Nehemia 8:13)

7. Kulingana na Kumbukumbu la Torati 21:20, 21, mwana mshupavu angeuawa kwa kupigwa mawe kwa sababu ya matendo gani?

8. Buli, mwezi wa nane katika kalenda takatifu ya Wayahudi, unajulikana kwa mambo gani tofauti yanayohusiana na ibada ya Waisraeli? (1 Wafalme 6:38; 12:26-33)

9. Ni bidhaa gani ya kawaida iliyokuja kuwa alama ya uthabiti na hali ya kudumu? (Hesabu 18:19)

10. Ni nini kilichomjulisha kaka wa mwana mpotevu kuwa kuna jambo lisilo la kawaida nyumbani? (Luka 15:25)

11. Malaika wa saba alimwaga wapi bakuli lake la hasira ya Mungu? (Ufunuo 16:17)

12. Ni upi uliokuwa mpaka wa mashariki wa milki ya Mfalme Ahasuero wa Uajemi? (Esta 1:1)

13. Katika maono, Yohana aliwaona nani wakiwa wameketi kwenye viti vya ufalme kuzunguka kiti cha ufalme cha Yehova? (Ufunuo 4:4)

14. Yesu aliwaita nini Mafarisayo wapenda-mapokeo? (Mathayo 15:14)

15. Watu wa kale waliiitaje bahari ya Mediterania tangu wakati wa Musa na kuendelea? (Hesabu 34:6)

16. Yule towashi Mwethiopia alikuwa akifanya nini Filipo alipokaribia gari lake? (Matendo 8:28)

17. Ni jambo gani lilifanywa iwapo mtumwa Mwebrania angekataa kuwekwa huru na bwana wake? (Kutoka 21:6)

18. Yule Msamaria mwema alimpeleka wapi yule Mwisraeli aliyemkuta barabarani akiwa nusura kufa? (Luka 10:34)

19. Ni nani aliyekuwa mfalme wa kwanza mwadilifu kutawala ufalme wa Yuda? (1 Wafalme 15:11)

20. Ni nani aliyekuwa msanii na mjenzi mkuu wa tabenakulo, na msaidizi wake mkuu alikuwa nani? (Kutoka 31:2-6)

21. Yesu ana uhusiano wa aina gani na kutaniko la Kikristo, unaokazia ukichwa wake na upendo wake? (Waefeso 5:22, 23; Ufunuo 21:2)

22. Ni mwanamke yupi mashuhuri aliyemsikiliza Paulo akijitetea kwenye Areopago na hatimaye akawa Mkristo? (Matendo 17:33, 34)

23. Gavana Festo alisema kwa sauti kubwa kwamba ‘kusoma kwingi’ kulimwongoza Paulo kuwa katika hali gani? (Matendo 26:24)

24. Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangwe kuu akiwa amepanda mnyama yupi? (Yohana 12:14, 15)

Majibu ya Maswali

1. Malimbuko ya mazao

2. Jembe

3. Kuchonga mawe

4. Kleopasi

5. Hamu

6. Ezra

7. Ulafi na ulevi

8. Solomoni alikamilisha ujenzi wa hekalu, Yerusalemu; na Yeroboamu kwa ushupavu akafanya msherehekeo katika mwezi huo ili kukengeusha watu katika ufalme wa kaskazini wasihudhurie sherehe zilizokuwa Yerusalemu

9. Chumvi

10. “Alisikia utumbuizo wa kimuziki na uchezaji-dansi”

11. “Juu ya hewa”

12. India

13. Wazee 24

14. “Viongozi vipofu”

15. Bahari Kuu

16. Akisoma unabii wa Isaya

17. Sikio lake lilitobolewa kwa uma

18. Kwenye hoteli ndogo

19. Asa

20. Bezaleli, Oholiabu

21. Mume

22. Damarisi

23. Kunamsukuma kuingia katika kichaa

24. Mwana wa punda