Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kelele ya Theluji

Kelele ya Theluji

Kelele ya Theluji

WANASAYANSI wamegundua kwamba theluji inapoanguka kwenye maji, kila kipande kidogo cha theluji hutoa sauti isiyosikika na mwanadamu. Sauti hiyo iliyo kama king’ora cha gari la zima-moto hufikia kilele na kufifia kwa haraka sana.

Tone la mvua au jiwe la mvua hutumbukia majini, lakini kipande chepesi cha theluji huelea juu. Lakini baada ya muda mfupi huyeyuka na “mlio,” unaotajwa hapo juu, hutokea. Jambo hilo liligunduliwa yapata miaka 15 iliyopita, lakini ugunduzi huo haukutiwa maanani. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, sauti hizo zimekuwa zikitatiza vyombo vinavyotumiwa na wanabiolojia kufuata nyendo za samaki aina ya salmoni wanapohama huko Alaska. Kelele hiyo ya theluji inapokatiza ishara kutoka kwa samaki, shughuli ya kuwafuatia samaki hao hulazimika kusimamishwa. Jambo hilo hutokezwa na nini?

Gazeti New Scientist lasema kwamba vipande vya theluji vinapokuwa vikielea juu ya maji, hutokeza kelele kidogo majini. Lakini, mara tu vianzapo kuyeyuka, maji hufyonzwa. Yawezekana kwamba povu hutoka wakati huo kwenye vipande hivyo vya theluji au hubanwa na maji yanayopanda. Kila povu huyumbayumba ili kufaana na hali ya mazingira yake, na kwa kufanya hivyo, hutoa wimbi la sauti, ambalo lafanana na mlio wa kengele—lakini lenye sauti kubwa zaidi.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Snow Crystals/Dover