Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mzambarausime Nataka kuwashukuru kwa ajili ya makala “Mzambarausime—Ua Lisilo la Kawaida Lenye Uzuri wa Kupendeza.” (Februari 22, 2000) Nafurahia ziara za washiriki wa kanisa lenu, ingawa sidhani kamwe kama nitajiunga na dini yao. Hata hivyo, makala hiyo iliandikwa na mtu anayefahamu vyema mzambarausime. Katika ulimwengu huu wenye matatizo, kukuza mzambarausime ni njia nzuri ajabu ya kustarehe na kufurahia maisha.

C. M., Marekani

Kujiua Ule mfululizo wa makala “Kujiua—Ni Nani Walio Hatarini Zaidi?” (Februari 22, 2000) ulitusaidia sana. Miezi minane iliyopita mama yangu alikufa ghafula. Baba hakuwa nyumbani wakati huo na yeye hujilaumu. Yeye husema kwamba hana tamaa ya kuishi. Kwa hivyo, makala hayo yalikuwa yenye kunifaa sana mimi na baba yangu.

R. Z., Ujerumani

Babu yangu alijiua miaka miwili iliyopita. Baada ya mke wake kufa, hali yake ya kiakili ilidhoofika sana. Makala zenu zilinisaidia nielewe kwa nini babu alijiua.

A. M., Marekani

Mnamo Januari ndugu yangu mwenye umri wa miaka 48 alijiua. Siku moja baada ya hotuba ya mazishi, baba yangu ambaye si mmoja wa Mashahidi wa Yehova, alipata toleo hilo la Amkeni! kwenye sanduku letu la barua. Alikuwa ameshikwa na bumbuazi huku akitokwa na machozi alipokuwa akituonyesha toleo hilo. Familia yetu ilikuwa ikitokwa na machozi ya shangwe na shukrani kwa ajili ya mfululizo huo wenye kufariji.

B. J., Marekani

Kwenye shule zilizo katika wilaya yetu, watoto sita walijiua mwaka jana. Hali hii imekuwa yenye kuhangaisha sana hivi kwamba shule zote katika wilaya zimetahadharishwa kuhusu tatizo hilo la kujiua. Tulitoa toleo hili kwa watu walio kwenye maeneo ambayo kwa kawaida hayapendezwi na ujumbe wetu. Nyakati nyingine watu waliyachukua magazeti hayo kutoka mikononi mwetu hata kabla hatujamaliza utangulizi wetu!

C. C., Marekani

Nilipokuwa kijana, nilijaribu mara mbili kujiua baada ya kifo cha baba yangu. Neno lenyewe “kujiua” ni mwiko kwa baadhi ya watu. Asanteni sana kwa kuliweka kwenye jalada la Amkeni! Nilipata makala hizo zikiwa wazi, halisi, na zenye kuelewa hali sana.

M. G., Ufaransa

Matatizo ya Urafiki Makala“Vijana Huuliza . . . Kwa Nini Rafiki Yangu Aliniumiza?” (Februari 22, 2000) ilinisaidia. Rafiki yangu wa karibu sana kwa muda wa miaka sita na nusu aliniumiza sana. Tukitumia madokezo katika makala hiyo yenu, mimi na rafiki yangu tulizungumzia tatizo letu kwa amani na kwa utulivu. Tokeo ni kwamba tumekuwa marafiki wa karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

M. L., Marekani

Mhubiri Aliye Mlemavu Makala “Wakati Ujao Wenye Tumaini Licha ya Udhaifu” (Februari 22, 2000) ilinigusa sana. Mimi ni mchanga, na nyakati nyingine mimi huona matatizo yangu kuwa yasiyoweza kushindwa. Simulizi la Konstantin Morozov lilikuwa lenye kutia moyo sana. Nathamini sana maneno haya yake: “Nataka kuendelea kumtumikia [Yehova] maadamu moyo wangu unaendelea kupiga.”

L. C., Italia

Nina watoto watatu, na kwa kuwa mume wangu hashiriki imani yangu, ni daraka langu kuwafundisha mambo ya kiroho. Nafanya kazi ya kuajiriwa na pia nahitaji kutunza nyumba, kwa hiyo nyakati nyingine huwa nimechoka sana. Mtazamo chanya wa Konstantin ni wa ajabu sana! Asanteni sana kwa kuchapisha simulizi lake.

O. K., Urusi