Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 23. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Waisraeli waliposhindwa katika Ai kwa sababu ya kuvunja maagizo ya Mungu kuhusu Yeriko na kukawa hakuna mtu aliyekiri dhambi hiyo, mkosaji alifunuliwaje? (Yoshua 7:14-21)

2. Kwa nini Yehova alimwua Onani mwana wa Yuda? (Mwanzo 38:7-10)

3. Ni nani aliyemkemea Hana mwadilifu kwa kudhani alikuwa mlevi? (1 Samweli 1:13, 14)

4. Kwa sababu gani Yesu alisema kwamba waandishi “watapokea hukumu nzito zaidi”? (Luka 20:46, 47)

5. Ni nani aliyeandika vitabu viwili vya Mambo ya Nyakati? (Nehemia 12:26)

6. Ni nini kinachowakilisha kitamathali uwezo au nguvu katika Biblia? (Yeremia 32:17)

7. Kipimo cha shamba ambacho jozi ya fahali wangelima kwa siku moja chaitwaje katika Biblia? (1 Samweli 14:14, Biblia Habari Njema)

8. Negebu inapatikana wapi? (Kutoka 26:18)

9. Wamisri, Waethiopia, na Wakanaani ni wazao wa mwana yupi wa Noa? (Mwanzo 10:6)

10. Solomoni alikamilisha ujenzi wa hekalu mwezi gani? (1 Wafalme 6:38)

11. Ni mmea upi uliotimiza fungu muhimu katika ushindi wa Daudi dhidi ya Wafilisti katika bonde la Warefai? (2 Samweli 5:24)

12. Ni njia gani nyingine ya ziada anayotumia yule mpanda-farasi wa nne wa Ufunuo kuvuna wahasiriwa wake? (Ufunuo 6:8)

13. Kwa sababu gani Wanefili waliitwa “watu wenye sifa”? (Mwanzo 6:4)

14. Kwa amri ya Yehova, ni nini lililofanywa ili watu wa vizazi vya baadaye waweze kuona mana waliyoila Waisraeli nyikani? (Kutoka 16:32, 33)

15. Timotheo alijua nini “tangu utoto sana” ambayo yangemfanya awe “mwenye hekima kwa ajili ya wokovu”? (2 Timotheo 3:15)

16. Ni nani walioondoa miili ya Sauli na wanae ukutani kwa Beth-shani, ilipokuwa imeangikwa na Wafilisti, na kuizika kwa heshima? (1 Samweli 31:11-13)

17. Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana walikuwa wapi Yesu alipowaita wawe wafuasi wake? (Mathayo 4:18-22)

18. Ni mfalme yupi wa Ashuru aliyepewa ushuru na Menahemu, mfalme wa Israeli, ili asishambulie Israeli? (2 Wafalme 15:19)

Majibu ya Maswali

1. Yehova aliweka taifa kwenye jaribu, akachagua kwanza kabila, kisha jamaa, kisha nyumba, kisha yule mwanamume Akani

2. Kwa kumkaidi baba yake na kuwa mwenye wivu, Onani alizuia ndugu yake Eri aliyekufa kupata mrithi

3. Kuhani mkuu Eli

4. Kwa sababu waling’ang’ania umashuhuri, na kwa pupa ‘walimeza nyumba za wajane,’ nao walisingizia utakatifu kwa kutoa sala ndefu

5. Ezra

6. Mkono

7. “Ekari”

8. Kusini

9. Hamu

10. Buli

11. Mforsadi

12. Kwa “tauni ya kufisha”

13. Hurejezea, si sifa kuhusiana na Mungu, bali ni hofu waliyoeneza wakiwa wachokozi na wakatili

14. Kopo lilijazwa pishi moja ya mana na kuwekwa “mbele ya BWANA”

15. “Maandishi matakatifu”

16. Wanaume mashujaa wa Yabesh-gileadi

17. Bahari ya Galilaya

18. Pulu (Tiglathi-pileseri wa tatu)