Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Karne ya Ishirini Hongera kwa kazi mnayofanya ya kuarifu na kuelimisha. Nikiwa mleta-habari wa mambo ya kisiasa na ya kijeshi, daima mimi huwa mchambuzi wa makala ninazosoma. Lakini mfululizo wa makala “Karne ya 20—Miaka Muhimu ya Badiliko” ulikuwa bora zaidi. (Desemba 8, 1999) Picha ya jalada ilionyesha wazi matukio muhimu sana ya karne hiyo.

A. P., Angola

Melatonini na Mshuko-Moyo Nilivutiwa na makala “Usiku Mrefu” katika “Kuutazama Ulimwengu.” (Machi 8, 2000) Ninafanya kazi katika taasisi ambayo inachunguza melatonini, na inaonekana kuwa maelezo yenu yalikuwa na makosa. Ikiwa melatonini inahusika katika mshuko-moyo wa majira, basi ni wingi wake kuliko upungufu wa homoni hiyo unaosababisha hali hiyo.

X. Y., Ufaransa

Sasa inaonekana kwamba uhusiano hususa kati ya melatonini na mshuko-moyo wa majira—iwapo upo—haujahakikishwa. Hivi karibuni wachunguzi wamedokeza kwamba huenda suala linalohusika si kiwango cha melatonini, bali jinsi ukosefu wa nuru unavyoathiri kutokezwa kwa melatonini. Kwa wazi, uchunguzi zaidi wahitajika kabla ya uamuzi hakika kufanywa.—Mhariri.

Kasoro ya Usanii? Nilikuwa hospitalini na nikawa nasoma toleo la Januari 8, 2000, lenye mfululizo wa makala kuu “Tiba na Upasuaji Bila Damu—Uhitaji Unaoongezeka,” kisha akaingia mtaalamu mkuu wa moyo akiandamana na kikundi cha wanafunzi. Yeye alisema kwamba picha ya EKG (picha ya kadiogramu) inatazama upande wa nyuma.

J. T., Uingereza

Picha hiyo ilikuwa ya kisanii. Ilichunguzwa na wataalamu wa kitiba kabla ya kuchapishwa; hata hivyo, maoni ya ujumla ya wataalamu wengine wa kitiba ambao wameiona picha hiyo tangu ichapishwe ni kwamba ilichorwa kimakosa. Twaomba radhi kwa kosa hilo.—Mhariri.

Kuacha Kuvuta Sigareti Hadi hivi karibuni nimekuwa mraibu wa sigareti, bangi, kileo, na kokeini. Nilijaribu mara nyingi kuacha bila kufanikiwa. Nilipoanza kujifunza Biblia na mmoja wa Mashahidi wa Yehova ndipo tu nilipoanza kujistahi. Kwa msaada wa Yehova, sijatumia dawa zozote za kulevya wala kuvuta sigareti tangu Januari. Nimesumbuliwa sana na dalili za kuacha. Tangu Januari nimekuwa na tatizo la kukosa usingizi. Mfululizo wa makala “Jinsi Unavyoweza Kuacha Kuvuta Sigareti” katika toleo la Machi 22, 2000, ulinisaidia kuona kwamba tatizo langu la kukosa usingizi ni mojawapo ya dalili za kuacha wala si kwamba nimeshikwa na kichaa! Asanteni sana.

D. M., Marekani

Niliposoma maelezo yenu kuhusu dalili za kuacha nikotini, ilinikumbusha kisa changu. Mwanzoni sikuweza kuwazia jambo jingine ila sigareti. Hatimaye siku, kisha majuma, kisha miezi ikapita bila wazo la sigareti kuja akili ni mwangu. Pasipo shaka, Yehova alinisaidia baada ya kuazimia binafsi kwamba sitavuta sigareti tena kamwe. Hiyo ilikuwa miaka 20 iliyopita, na kwa kweli sijavuta sigareti tena kamwe.

D. A., Italia

Nondo Asanteni sana kwa kuchapisha makala “Upendo Unaposhindwa Kuona,” kuhusu nondo-maliki. (Machi 22, 2000) Nilimwona mmoja kwenye bustani yangu. Nondo mwingine alipojiunga naye, nilipiga picha iliyoonyeshwa katika televisheni ya hapa kwetu. Nathamini sana kazi ngumu na utafiti unaohusika katika kuandaa magazeti haya.

I. K., Marekani

El Niño Nataka kuwashukuru kwa ajili ya makala yenye kuarifu “El Niño Ni Nini?” (Machi 22, 2000) Kwa kweli, nilisikia mengi kuhusu El Niño katika mwaka wa 1998, lakini sikuwahi kuelewa maana yake. Maelezo yake yaliletwa hadi mlangoni pangu! Makala yenu ilikuwa fupi lakini yenye kuarifu kwelikweli.

U. N., Marekani