Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 19. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)

1. Huko nyikani, ni usemi gani uliotumika kwa makazi ya Musa na maskani [tabenakulo] takatifu? (Kutoka 33:7; 39:40)

2. Hekalu la Artemi lililoonwa kuwa mojawapo ya maajabu saba ya ulimwengu wa kale, lilikuwa wapi? (Matendo 19:26, 27)

3. Ofisa Mbabiloni aliyekuwa chini ya amiri alikuwa na cheo gani? (Danieli 2:48)

4. Chini ya Sheria ya Kimusa, Walawi walihitaji kupewa sehemu gani, na kwa nini? (Kumbukumbu la Torati 26:12)

5. Ni nani aliyekuwa kahaba hapo awali ambaye alikuja kuwa nyanya wa kale wa Yesu? (Mathayo 1:5)

6. Paulo alipata kujuana na Akila na Prisila katika jiji gani? (Matendo 18:1-3)

7. Ni “urembo” gani ambao Petro anapendekeza kwa wanawake Wakristo? (1 Petro 3:3, 4)

8. Ni kazi gani ambayo lazima ifanywe kabla mwisho wa mfumo huu wa mambo kuja? (Mathayo 24:14)

9. Jina Kaisari lilikuwa cheo cha kifalme kilicholingana na cheo gani?

10. Ni sehemu gani muhimu ya silaha za kiroho za Mkristo ambayo humwezesha “kuzima vishale vyote vinavyowaka moto vya yule mwovu”? (Waefeso 6:16)

11. Meli ziliendeshwa kwa kutumia nini nyakati za kale? (Ezekieli 27:6, 7, 29)

12. Ni nini ambacho hakikuwa sehemu ya mlo wa mwanadamu kabla ya Gharika? (Mwanzo 9:3, 4)

13. Ni kitu gani kisichopenya maji kilichotumiwa kufunika safina? (Mwanzo 6:14)

14. Ni nini ambacho Yesu alikiita “udanganyifu,” kiwezacho kulisonga neno la Ufalme na kumwacha mtu akiwa “asiyezaa matunda”? (Mathayo 13:22)

15. Petro alisema kungekuwa na matokeo gani iwapo mtu angejitakasa nafsi yake kwa “kutii ile kweli”? (1 Petro 1:22)

16. Katika safari yake ya pili ya mishonari, Paulo alienda wapi ‘alipokatazwa na roho takatifu asiseme neno katika wilaya Asia’? (Matendo 16:6)

17. Ni kiambishi gani, kinachomaanisha “mwana,” kinachopatikana mara nyingi katika majina ya Kiebrania? (Mwanzo 35:18)

18. Mfalme Uzia alipatwa na nini baada ya kufukiza uvumba hekaluni kwa kimbelembele? (2 Mambo ya Nyakati 26:19-21)

19. Kwa kawaida vazi rasmi la nabii lilitengenezwa na nini? (2 Wafalme 1:8; Mathayo 3:4)

20. Ni Kaisari yupi ambaye kwa wazi aliagiza Paulo auawe?

21. Ni mtu yupi ambaye anaripotiwa kihususa kuwa wa kwanza kutumia jina la Mungu? (Mwanzo 4:1)

Majibu ya Maswali

1. “Hema ya kukutania”

2. Efeso

3. Liwali

4. Zaka, au sehemu ya kumi. Kwa sababu hawakuwa na urithi nchini lakini walikuwa wametolewa kwa ajili ya utumishi wa patakatifu

5. Rahabu

6. Korintho

7. “Roho ya utulivu na ya upole”

8. “Habari njema ya Ufalme” lazima ihubiriwe duniani kote

9. Maliki

10. “Ngao kubwa ya imani”

11. Matanga na makasia

12. Nyama ya mnyama

13. Lami

14. ‘Nguvu za mali’

15. “Shauku ya kidugu isiyo na unafiki”

16. “[Ku]pitia Frigia na nchi ya Galatia”

17. Ben

18. Yehova alimpiga kwa ukoma

19. Manyoya ya ngamia au manyoya ya mbuzi

20. Nero

21. Hawa