Pambano Langu na Ugonjwa Wenye Kudhoofisha
Pambano Langu na Ugonjwa Wenye Kudhoofisha
KAMA ILIVYOSIMULIWA NA TANYA SALAY
Hadi miaka michache tu iliyopita, nilikuwa mama mwenye shughuli nyingi na mtumishi wa wakati wote katika mji huu mdogo wa Luverne, Alabama. Hali ya maisha huku ni tulivu na ya polepole. Maisha yalikuwa mazuri kwangu na kwa mume wangu, Duke, na mwana wangu mdogo, Daniel. Kisha upasuaji wa kawaida ukabadili maisha yetu kabisa.
MATATIZO yetu yalianza mwaka wa 1992, tumbo langu la uzazi lilipoondolewa. Punde baadaye, nilianza kuwa na maumivu makali yenye kuendelea na kukojoa mara nyingi (mara 50 hadi 60 kwa siku). Mwishowe daktari wangu wa magonjwa ya kina mama alipanga nimwone daktari wa mfumo wa mkojo ili kujaribu kujua kiini cha tatizo hilo.
Nilikwenda hospitalini nipimwe. Katika ziara yangu ya kwanza, daktari wa mfumo wa mkojo alitambua ugonjwa wangu—interstitial cystitis (IC), au uvimbe wa kibofu cha mkojo unaoathiri sehemu nyingine zilizoungana na kibofu. Haikuwa rahisi kutambua ugonjwa wangu kwa sababu dalili za ugonjwa huo zafanana na magonjwa mengine ya mfumo wa mkojo. Zaidi ya hayo, hakuna njia maalum ya kupimia ugonjwa huo. Kwa hiyo, lazima madaktari wafutilie mbali uwezekano wa magonjwa mengine kabla ya kukubali kuwapo kwa ugonjwa wa IC.
Daktari wetu alisema wazi kwamba, kwa kuwa hakuna matibabu yanayofanya kazi, hatimaye kibofu cha mkojo lazima kiondolewe! Alisema kwamba matibabu mengine yapo lakini hayana mafanikio. Bila shaka, habari hiyo ilikuwa pigo kwetu. Hadi wakati huo, nilikuwa nimekuwa mwenye afya nzuri. Kama Mashahidi wa Yehova, mimi na Duke tulikuwa tumetumikia katika huduma ya wakati wote kwa muda wa miaka kadhaa, na sasa niliambiwa kwamba kibofu changu cha mkojo lazima kiondolewe. Nashukuru kwamba mume wangu alinisaidia sana.
Tuliamua kumwona daktari mwingine wa mfumo wa mkojo. Tuliwaona madaktari kadhaa. Kwa kusikitisha, wakati huo madaktari wengi hawakuwa na ujuzi mwingi kuhusu ugonjwa huo. Pia, madaktari wengi wa mfumo wa mkojo wana nadharia zao wenyewe kuhusu ugonjwa wa IC, kwa hiyo matibabu yanayopendekezwa hutofautiana. Jarida moja la kitiba lasema: “Mara nyingi ugonjwa huo ni wa kudumu.” Jarida lingine lasema: “Wanasayansi hawajavumbua matibabu ya interstitial cystitis, wala hawajui ni matibabu gani yatakayomfaa mgonjwa fulani. . . . Kwa kuwa madaktari hawajui kile kinachosababisha ugonjwa huo, matibabu ni ya kutuliza maumivu tu.”
Nilikuwa na maumivu makali sana kwa sababu ya mkakamao na kukojoa mara nyingi hivi kwamba nilikuwa tayari kujaribu chochote kile walichopendekeza madaktari. Nimejaribu dawa 40 mbalimbali na vilevile mitishamba, tiba ya vitobo, nusukaputi ya neva fulani za mwili, kudungwa sindano ya utando wa nje wa uti wa mgongo na sindano ya uti wa mgongo. Na pia matibabu ya transcutaneous electrical nerve stimulation, (TENS), ambayo huhusisha mipwito midogo ya umeme ya kuchochea neva inayopitishwa mwilini kupitia ngozi kwa muda wa dakika au saa kadhaa. Nilifanya utafiti kwa kadiri nilivyoweza, nao ukanisaidia angalau kuelewa kwa kiasi fulani ugonjwa huo.
Kwa sasa, natumia methadone, ambayo ni dawa ya kutuliza maumivu, pamoja na dawa nyingine sita. Pia, huwa ninakwenda kwenye kituo cha afya cha kutuliza maumivu ambapo mimi huchomwa sindano ya utando wa nje wa uti wa mgongo na vilevile kupewa steroidi ili kutuliza maumivu. Ili kupunguza kukojoa mara nyingi, ninakwenda hospitalini kila baada ya miezi mitatu au minne kwa matibabu ya kupanua kibofu cha mkojo kwa kutumia umajimaji. Nimetibiwa kwa njia hiyo mara kadhaa. Kwa ukawaida matibabu hayo hunisaidia kwa muda wa miezi kadhaa. Nimelazwa hospitalini zaidi ya mara 30 katika miaka michache iliyopita.
Vipi matibabu ya mwisho, kuondolewa kwa kibofu cha mkojo? Kitabu kimoja chasema: “Madaktari wengi husita kufanya upasuaji huo kwa sababu tokeo la mgonjwa mmoja-mmoja halitabiriki—baadhi ya wagonjwa wanaopasuliwa wanaendelea kuwa na matatizo.” Kwa hiyo, kwa sasa siufikirii upasuaji.
Nyakati nyingine maumivu ni makali na ya kuendelea hivi kwamba ingekuwa rahisi kukata tamaa. Hata nimewahi kufikiria kujiua. Lakini nilifadhaishwa na wazo la jinsi tendo la aina hiyo lingetia suto jina la Yehova. Naweza kuona umuhimu wa sala na funzo la kibinafsi na vilevile wa kuwa na uhusiano wa karibu na Yehova, kwa kuwa hatujui kinachoweza kutukia na kubadili maisha yetu. Uhusiano wa karibu pamoja na Yehova umeokoa maisha yangu nilipokuwa mgonjwa, la sivyo ningekuwa nimejiua.
Mhubiri 12:1, lisemalo hivi: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo.” Ninashukuru kwamba nilianza kufanya utumishi wa wakati wote nilipokuwa na umri wa miaka 15 na kuweza kuendelea kwa muda wa miaka 20 hivi. Wakati huo nilisitawisha uhusiano wa karibu na Yehova.
Ninapofikiria miaka hiyo tisa naona jinsi maisha yawezavyo kubadilika haraka. Naelewa maana ya maneno yaNinamshukuru Yehova kwa mume wangu na mwana wangu Daniel, ambao wamenisaidia. Pia ninatiwa moyo sana akina ndugu na dada wa kutaniko wanaponipigia simu au kunitembelea. Siwezi kutoka sana wakati wa majira ya baridi kali kwa kuwa baridi huzidisha mkakamao. Kwa hiyo, wakati wa baridi natoa ushuhuda kupitia simu, na jambo hilo lanisaidia kushikilia tumaini la Paradiso na kulidumisha kuwa halisi kwangu. Natazamia wakati magonjwa na mateso yatakapokuwa yamepita na hayatakumbukwa tena.—Isaya 33:24.