Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Watafua Panga Zao Ziwe Majembe”—Lini?

“Watafua Panga Zao Ziwe Majembe”—Lini?

“Watafua Panga Zao Ziwe Majembe”—Lini?

SANAMU maarufu ya mwanamume afuaye panga liwe jembe yasimama kwenye ua wa Umoja wa Mataifa jijini New York City. Imechongwa kwa kupatana na unabii wa Biblia wa Isaya sura ya 2, mstari wa 4, na Mika sura ya 4, mstari wa 3. Maneno hayo yatatimizwa lini na jinsi gani?

Ripoti ya karibuni katika gazeti la The New York Times ilikuwa na kichwa kilichosema “Mauzo ya Silaha Duniani Yamepanda Kufikia Dola Bilioni 30 za Marekani”! Ni nchi zipi hasa zilizouza silaha hizi zote mwaka wa 1999? Marekani iliongoza kwa mauzo ya dola bilioni 11.8 za Marekani. Urusi ilikuwa ya pili kwa mauzo yaliyopungua nusu ya yale ya Marekani. Hata hivyo, mauzo ya Urusi yalikuwa karibu maradufu ya mauzo yake ya mwaka uliotangulia. Nchi za Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza, na Italia zilifuata. Ripoti iyo hiyo ilisema: “Kama zamani, theluthi mbili ya silaha zote ziliuziwa nchi zinazoendelea.”

Baada ya vita viwili vya ulimwengu na vita vikubwa vingine vingi vya karne ya 20, ambavyo viliua na kujeruhi mamilioni, mtu aweza kuuliza, “Je, mataifa yatajifunza amani badala ya vita wakati wowote?” Biblia yadokeza kwamba yatajifunza amani “katika siku za mwisho.” (Isaya 2:2) Kwa hakika, unabii huo tayari unatimizwa, kwa maana Mashahidi wa Yehova karibu milioni sita wamekubali ‘kufundishwa na BWANA.’ Kwa sababu hiyo, ‘amani yao ni nyingi.’—Isaya 54:13.

Hivi karibuni Yehova atamaliza silaha na vita vyote na wanaoviendeleza, kwa kuwa ‘atawaangamiza wale wanaoangamiza dunia.’ Ukitaka kupata habari zaidi kuhusu badiliko hilo la ajabu, jisikie huru kuwasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lako au tumia anwani ifaayo kwenye ukurasa wa 5.—Ufunuo 11:18.