Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Santeria Mwaanza makala yenu ya Amkeni! ya “Uvutio wa Santeria” (Julai 8, 2000) kwa kudokeza kwamba Santeria ni dini maarufu ya Kuba hasa, na kwamba kutoka Kuba ilienea hatua kwa hatua kufikia nchi nyingine. Hata hivyo, ndani ya makala, tunaweza kuona kwamba Santeria ilipelekwa na watumwa Waafrika kutoka Nigeria hadi visiwa vyote vya Karibea. Makala hiyo haikuandikwa na Mkuba bali na mtu wa Mexico. Uandishi wa aina hiyo unapotosha ukweli, nao unaharibu jina lenu.

V. R., Marekani

Hatukukusudia kusema kwamba Santeria ni “dini maarufu ya Kuba hasa.” Kinyume cha hilo, tulijaribu kuonyesha kwamba Santeria ni dini inayofuatwa sana katika sehemu nyingine za dunia, kutia ndani Mexico na Marekani. Kamusi ya “Encyclopædia Britannica” yasema kuhusu uenezi wa Santeria kwamba, Santeria ni “madhehebu yaliyoanza Kuba na kuenea hadi visiwa vya karibu . . . Chanzo chake ni mapokeo ya Wayoruba (wanaoishi leo nchini Nigeria na Benin).—Mhariri.

Endometriosis Asanteni sana kwa makala ya “Matatizo Yangu ya Endometriosis.” (Julai 22, 2000) Mimi pia nina ugonjwa wa endometriosis, nami nimeteseka sana. Baadhi ya ndugu zangu wa Kikristo hawakuelewa kwa nini nilikuwa mgonjwa sikuzote. Lakini baada ya kusoma makala hiyo, sasa wanaelewa.

G. S., Jamaika

Simulizi kuhusu Deborah Andreopoulus lilikuwa kama simulizi la maisha yangu mwenyewe! Nimeteseka kwa miaka mingi, na makala hiyo ilikuwa jibu kwa sala zangu. Ilinitia moyo sana.

J. C. F., Ireland

Miezi miwili na nusu iliyopita nilipata kujua kwamba nina ugonjwa wa endometriosis. Jambo linalonitia moyo sana ni kujua kwamba si mimi tu, bali kuna wanawake wengi walio na tatizo hilohilo.

A. W., Guatemala

Asanteni kwa kuzungumzia jinsi ambavyo ugonjwa huo huathiri si mgonjwa tu, bali pia marafiki na familia. Nilipoona makala yenu nilijua kwamba Yehova hutujali kwelikweli na huelewa matatizo tunayokabili.

N. A., Kanada

Bado siku chache na nitapasuliwa, na yale yaliyompata Deborah Andreopoulus yamenitia moyo. Sasa nafikiri ninaweza kukabili tatizo langu nikiwa na mtazamo unaofaa.

M. B., Italia

Antaktika Nimesoma mara nyingi makala ya “Antaktika—Mradi Mpya wa Mwisho” (Julai 22, 2000). Mwandishi wetu wa Amkeni! nchini Australia na msanii wa maandishi aliyeunda makala hiyo walifanya kazi nzuri ajabu! Makala hiyo ilinikumbusha mambo yaliyopita. Katika Mwaka wa Kimataifa wa Jiofizikia, yapata miaka 45 iliyopita, kikundi cha wanasayansi Wamarekani waligawiwa kazi ya kuchunguza Antaktika. Uchunguzi wao wote uliandikwa katika vitabu vikubwa vitatu. Kwa kuwa mimi ninafanya kazi yangu mwenyewe kama msanii wa maandishi, niliajiriwa kuunda vitabu hivyo. Leo mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, na nimekuwa mhubiri wa habari njema wa wakati wote kwa muda wa miaka 6. Kwa kuwa nina picha na ramani nyingi za Antaktika katika mahali pangu pa kazi, bado nimezungukwa na Antaktika. Asanteni kwa makala hiyo!

C. M., Marekani