Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 19. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Daudi alichukua hatua gani mwishowe ili kuficha dhambi aliyofanya pamoja na Bath-sheba? (2 Samweli 11:15-17)
2. Mwanamke wa kwanza aliumbwa kutokana na nini? (Mwanzo 2:22)
3. Petro aliyalinganisha matendo ya wale wanaoliacha “pito la uadilifu” na matendo ya wanyama gani? (2 Petro 2:21, 22)
4. Watu walianza “kuliitia Jina la BWANA” katika siku za nani? (Mwanzo 4:26)
5. Ni nani aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Israeli, na babake aliitwa nani? (Matendo 13:21)
6. Chini ya Sheria ya Kimusa, angalau mashahidi wangapi walihitajiwa ili mtu ahukumiwe kifo? (Kumbukumbu la Torati 17:6)
7. Paulo alisema “kila familia mbinguni na duniani hupata jina layo” kutoka kwa nani? (Waefeso 3:14, 15)
8. Yabali na Yubali, wana wa Lameki, wanajulikana sana kwa mambo gani? (Mwanzo 4:20, 21)
9. Kama vile Yakobo na Petro wanavyoonyesha, Mungu huwapa nani “fadhili isiyostahiliwa”? (Yakobo 4:6; 1 Petro 5:5)
10. Paulo atumia semi zipi kufananisha waovu na waadilifu katika mfano wake wa mfinyanzi na udongo wake? (Waroma 9:22-24)
11. Paulo alikata rufani kwa Kaisari yupi? (Matendo 25:11, 21)
12. Chini ya Sheria ya Kimusa, ni mambo gani mawili yaliyokuwa ya lazima ili mnyama awe kati ya wale safi na wanaofaa kuliwa? (Mambo ya Walawi 11:2, 3, Biblia Habari Njema)
13. Ni nini herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kiebrania? (Maandishi ya utangulizi ya Zaburi 119, NW)
14. Waisraeli walipaswa kufanya nini kwenye ncha za nguo zao ili kuwakumbusha kwamba walikuwa wametengwa kuwa watu walio watakatifu kwa Yehova? (Hesabu 15:38-41)
15. Abramu aliondoka kwenye jiji gani alipoelekezwa na Yehova aende Kanaani? (Mwanzo 15:7)
16. Kwa nini yule Farisayo aliyeitwa Simoni alichukizwa mwanamke alipoibusu miguu ya Yesu kwa wororo na kuipaka mafuta yenye marashi? (Luka 7:37-39)
Majibu ya Maswali
1. Alipanga Uria auawe vitani
2. Ubavu uliotwaliwa katika Adamu
3. Mbwa na nguruwe-jike
4. Enoshi
5. Sauli, Kishi
6. Wawili
7. “Baba,” Yehova Mungu
8. Wao ndio waliokuwa wa kwanza kati ya wafugaji wanyama wa kuhama-hama na wanamuziki
9. “Wanyenyekevu”
10. “Vyombo vya hasira ya kisasi” na “vyombo vya rehema”
11. Nero
12. Alipaswa kucheua na kuwa na kwato zilizogawanyika sehemu mbili
13. Aleph
14. Walipaswa kufanya vishada na kuvitia nyuzi ya rangi ya samawi
15. Uru wa Wakaldayo
16. Kwa sababu mwanamke huyo alijulikana kuwa mtenda-dhambi aliyeishi maisha ya ukosefu wa adili na bado Yesu alimruhusu amguse