Wako Karibu Kutoweka
Wako Karibu Kutoweka
SAM, sokwe wa miaka mitatu unayeona kwenye picha, anaonekana kuwa mwenye huzuni. Lakini jambo hilo halipaswi kutushangaza. Wawindaji walimwua mamake, na kumwacha yatima bila kuwa na matumaini ya kurudi msituni. Kwa kusikitisha, miezi michache baada ya picha hiyo kupigwa, Sam alikufa kutokana na ugonjwa wa kupumua. Lakini, si huyo sokwe mmoja tu aliyekosa matumaini ya kuokoka.
Uharibifu unaoendelea wa makao yao ya asili umehatarisha jamii hiyo ya sokwe. Na kwa kuwa katika sehemu fulani sokwe huuawa na kuliwa, wawindaji wenye bunduki za kisasa wanatisha uwezekano wa wanyama hao kuishi kwa muda mrefu. Japo sokwe wanaonekana kuwa hatarini, jamii nyingine za wanyama zimo hatarini hata zaidi.
Ripoti moja iliyotayarishwa na Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Viumbe na Mali za Asili (IUCN) inaonyesha jinsi wanyama-pori wengi ulimwenguni wanakabili hatari kubwa inayosikitisha. Katika miaka michache iliyopita, jamii nyingi zaidi za wanyama zimehatarishwa na nyingi zimetoweka haraka sana. Shirika la IUCN, linalochunguza hali ya maelfu ya jamii za wanyama, hivi majuzi lilichapisha Orodha ya Viumbe Walio Hatarini. Ilichapishwa ili kuwafahamisha watu zaidi kuhusu janga linalowakabili wanyama-pori wa dunia walio hatarini.
Robo moja hivi ya mamalia na sehemu moja kwa nane ya ndege wako karibu kutoweka. Na hizo ni jamii zilizorekodiwa tu. Hali ya jamii nyingi za wanyama duniani haijulikani.
Zaburi 50:10, Biblia Habari Njema) Basi hawezi kamwe kupuuza uharibifu mkubwa wa kazi yake. Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu atuhakikishia kwamba ‘atawaleta kwenye uangamizi wale wanaoiangamiza dunia.’—Ufunuo 11:18.
Ikiwa hali hiyo inakuhuzunisha, basi unafikiri Muumba wetu anahisije? Anasema hivi katika Neno lake, Biblia: “Wanyama wote porini ni mali yangu.” (Kulinda wanyama wa pori na mazingira ya dunia ambayo sisi sote hutegemea, ni mambo mawili tu kati ya kazi za haraka ambazo Ufalme wa Mungu utafanya wakati ‘Mungu atafanya vitu vyote kuwa vipya.’—Ufunuo 21:5; Mathayo 6:10.
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 16, 17]
Simba-milia (Panthera tigris)
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: 5,000 hadi 7,500 hivi (karne moja iliyopita walikuwa 100,000)
▪ Hatari kubwa: uwindaji-haramu, kutiliwa sumu, kupoteza makao, na umbali unaotenganisha jamii za simba-milia
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 17]
Giant Panda (Ailuropoda melanoleuca)
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: 1,000—ni mmojawapo wa wanyama wasiopatikana sana duniani
▪ Hatari kubwa: viwango vidogo vya uzalishaji na uharibifu wa misitu ya mwanzi wa milimani anayoitegemea kupata chakula
[Hisani]
▲ Foto: Zoo de la Casa de Campo, Madrid
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 17]
Orangutan (Pongo pygmaeus)
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: 20,000 hivi
▪ Hatari kubwa: moto msituni, ukataji-miti, uwindaji-haramu, na biashara ya magendo ya kuuza wanyama-vipenzi
[Hisani]
Foto: Zoo, Santillana del Mar, Cantabria, España ▼
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 18]
Lesser (Red) Panda (Panda Mwekundu) (Ailurus fulgens)
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: haijulikani, lakini idadi yao inaonekana inapungua kotekote katika mazingira yao kwa sababu wanadamu wanaharibu makao yao na vilevile kiwango kidogo cha uzalishaji
▪ Hatari kubwa: uwindaji-haramu, uharibifu wa misitu ya mwanzi wa milimani, uwindaji-haramu, na ulishaji wa mifugo
[Hisani]
Foto: Zoo de la Casa de Campo, Madrid
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 18]
Tumbili Aina ya Goeldi (Callimico goeldii)
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: haijulikani (mamalia huyu wa hali ya juu aligunduliwa mwaka wa 1904)
▪ Hatari kubwa: uharibifu wa msitu wa mvua wa Amazon na idadi ndogo ya wanyama wanaoweza kutawanyika kwa urahisi
[Hisani]
Foto: Zoo, Santillana del Mar, Cantabria, España
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 18]
Korongo Mwenye Kibwenzi Chekundu [Grus japonensis]
▪ Idadi iliyokadiriwa ya wanaoishi porini: 2,000 hivi
▪ Hatari kubwa: kugonga nyaya za nguvu za umeme, uharibifu wa maeneo ya kutagia mayai, na uchafuzi
[Hisani]
© 1986 Steve Kaufman