Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 19. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Wafuasi wa Yesu wanaofuata hatua zake wanapokea nini wanapotiwa mafuta na roho takatifu? (Waebrania 3:1)

2. Kwa nini Yehova alimwita mwana wa pili wa Hosea, ambaye mke wake Gomer alimzaa, jina lenye kuogofya la Lo-ammi? (Hosea 1:9)

3. Akiwa na hekima ya kimbingu mtu atatokeza sifa gani kwanza, kulingana na Yakobo? (Yakobo 3:17)

4. Nebukadreza alifanya nini mara baada ya Danieli kufasiri ndoto ya sanamu? (Danieli 2:46, 47)

5. Ni rangi gani ambazo zilitumiwa hasa katika hema ya kukutania na kwa mavazi ya makuhani? (Kutoka 28:6)

6. Mtunga-zaburi alijisikia kama ndege zipi alipoteswa na kujisikia mpweke? (Zaburi 102:6)

7. Ni lango gani ambalo Yesu alisema ni lazima mtu aingie ili apate ‘barabara inayoongoza kuingia katika uhai?’ (Mathayo 7:13, 14)

8. Kwa nini Musa alifunika uso wake alipowapa wana wa Israeli amri za Mungu? (Kutoka 34:35)

9. Kwa nini Daudi alimpa Amasa cheo cha Yoabu ili awe jemadari wa jeshi, ijapokuwa alikuwa amemwunga mkono Absalomu ili kumpinga Daudi? (2 Samweli 19:13)

10. Chakula cha mana ambacho Waisraeli walipewa kimwujiza kilishuka kutoka mbinguni pamoja na nini? (Hesabu 11:9)

11. Mafarisayo walijaribuje kumtega Yesu ili afanye tendo la kuchochea uasi dhidi ya serikali ya Roma? (Mathayo 22:15-21)

12. Yokebedi alimfichaje mtoto wake mchanga “mzuri,” aliyekuwa na umri wa miezi mitatu, na hivyo kuokoa maisha yake? (Kutoka 2:2-10)

13. Balaamu alimwelekeza Balaki afanye nini kwenye kila mojawapo ya vilele vitatu vya vilima? (Hesabu 23:1, 14, 29)

14. Ni wana wangapi wa Hamani waliouawa na Wayahudi kwenye ngome ya Shushani? (Esta 9:12)

15. Ni jambo gani lisilo la kawaida lililotukia wakati wanafunzi wa Yesu walipokutanika huko Yerusalemu katika siku ya Pentekoste 33 W.K.? (Matendo 2:2-6)

16. Yonathani alisema nini alipomweleza Sauli ni kwa nini Daudi hakuwapo wakati wa mlo? (1 Samweli 20:6)

17. Yohana anaona nini kwanza katika njozi yake ya kiunabii? (Ufunuo 1:12)

18. “Umati mkubwa” watangaza kwamba wanawiwa nini na Mungu na Mwana-Kondoo? (Ufunuo 7:9, 10)

19. Kulingana na Paulo, kusudi la Sheria ya Musa lilikuwa nini na Sheria hiyo ilipitishwa jinsi gani? (Wagalatia 3:19)

20. Taja vitu viwili ambavyo Waisraeli hawakuruhusiwa kula. (Mambo ya Walawi 3:17)

21. Kulingana na taarifa tuliyo nayo ni nani aliyetumia jina la Mungu mara ya kwanza? (Mwanzo 4:1, NW)

22. Ni ishara gani iliyoonyesha kwamba Mwisraeli katika taifa la Israeli la kale alichagua kubaki kuwa mtumwa? (Kumbukumbu la Torati 15:17)

23. Kwa nini Ezra aliamuru kufunga kwenye mto wa Ahava huko Babeli? (Ezra 8:21)

Majibu ya Maswali

1. “Mwito wa kimbingu,” ili wawe wafalme na makuhani pamoja na Yesu Kristo

2. Ili kuonyesha kwamba Yeye ametupilia mbali Israeli lililokosa imani

3. Usafi wa kiadili, au moyo safi

4. Alianguka kifudifudi, akamsujudia Daudi, na kumsifu Yehova

5. Rangi za samawi, zambarau, na nyekundu

6. Mwari na bundi

7. “Lango jembamba”

8. ‘Ngozi ya uso wake iling’aa’ baada ya Mungu kusema naye

9. Daudi alisema kwamba Amasa alikuwa “mfupa” wake na “nyama” yake

10. Umande

11. Kwa kumwuliza ikiwa “yaruhusika kisheria kumlipa Kaisari kodi ya kichwa”

12. Alimweka katika kisafina cha nyasi ambacho alikipaka sifa na lami, akakiweka kando ya Mto Nile ambapo binti Farao alimpata

13. Aliagizwa ajenge madhabahu saba na kutoa dhabihu ya ng’ombe mume na kondoo mume katika kila mojawapo ya madhabahu hizo

14. Kumi

15. Kelele ilitoka mbinguni, “ndimi kama kwamba za moto zikawa zenye kuonekana” juu ya kila mwanafunzi, na wanafunzi wote walijazwa roho takatifu na wakaanza kusema lugha tofauti

16. Alisema kwamba Daudi alikuwa amekwenda Bethlehemu kwa sababu ya dhabihu ya mwaka kwa ajili ya jamaa yake yote

17. Vinara saba vya taa vya dhahabu

18. Wokovu

19. Ili “kufanya mikiuko-sheria iwe dhahiri.” ‘Ilipitishwa kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi’

20. Mafuta na damu

21. Hawa

22. Sikio la mtumwa lilitobolewa kwa uma

23. Ili wale waliorudi waweze kujinyenyekeza mbele za Yehova na kutafuta “njia iliyonyoka” kutoka kwake