Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 20. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Kulingana na Petro, ni mambo yapi ‘yanayoendesha pambano dhidi ya nafsi’? (1 Petro 2:11)
2. Mfalme Nebukadreza alisema nini kumhusu Yehova wakati aliporudishiwa utimamu wa akili? (Danieli 4:34, 35)
3. Kwa nini Yesu ‘hakuacha yeyote achukue chombo kupitia hekalu’? (Marko 11:16)
4. Mfalme Senakeribu wa Ashuru alimdhihaki Mfalme Hezekia wa Yuda kwa njia gani? (2 Wafalme 18:23)
5. Yesu aliwatia watu moyo wafanye nini badala ya kutoa viapo bila kufikiri? (Mathayo 5:37)
6. Kulingana na Sheria ya Musa, ni nini kilichopasa kufanywa kwa mtu aliyependekeza ibada ya miungu mingine, hata ikiwa alikuwa mtu wa jamaa? (Kumbukumbu la Torati 13:6-10)
7. Yehova alimwahidi Abrahamu kuwa hataharibu Sodoma na Gomora ikiwa angalau watu wangapi waadilifu wangepatikana huko? (Mwanzo 18:32)
8. Mfalme Sauli alikufa kwa njia gani? (1 Samweli 31:3, 4)
9. Kwa nini Uza aliuawa alipojaribu kuzuia Sanduku la Agano lisianguke? (Hesabu 4:15, 19, 20; 2 Samweli 6:6, 7)
10. Ni jiji gani la Makedonia lililopewa jina la mungu-jua wa Ugiriki? (Matendo 17:1)
11. Ni usemi upi wa Biblia unaowakilisha upande wa mashariki? (Ufunuo 16:12)
12. Daudi alitawala Israeli kwa miaka mingapi?
13. Yesu alikuwa akipumzika wapi alipozungumza na yule mwanamke Msamaria? (Yohana 4:6)
14. Kwa nini ni lazima mtu ‘aepuke kabisa semi tupu ambazo huhalifu lililo takatifu’? (2 Timotheo 2:16)
15. Wana watatu wa Noa waliitwa nani? (Mwanzo 10:1)
16. Kati ya wale mashujaa Wagadi 11 ‘waliojitenga kumfuata Daudi’ huko nyikani, ni nani aliyesemwa kuwa ‘alilingana na watu elfu’? (1 Mambo ya Nyakati 12:8-14)
17. Yesu alisema nini kwa huruma wanafunzi wake walipolala na hivyo kushindwa kumtegemeza usiku ambao alisalitiwa? (Marko 14:38)
18. Yesu alikuwa wa ukoo wa mfalme yupi wa Israeli? (Waroma 1:3)
19. Ni wanawake gani wanne wanaotajwa waziwazi kuwa walienda kwenye kaburi la Yesu ili kuupaka mwili wake manukato? (Marko 16:1; Luka 24:10)
Majibu kwa Maswali
1. “Tamaa za kimwili”
2. Mamlaka yake ni “ya milele,” na hakuna anayeweza kumzuia asitimize kusudi lake
3. Kwa sababu walikuwa wanatumia ua wa hekalu kama njia ya mkato kuelekea kwenye sehemu nyingine za jiji
4. Alitaka kumpa farasi 2,000 ili ionekane kama angeweza kupandisha watu juu yao
5. ‘Waache tu neno lao Ndiyo limaanishe Ndiyo, La yao, La’
6. Alipaswa auawe
7. Kumi
8. Baada ya kuumizwa vibaya na mishale ya Wafilisti, alijiua kwa kuangukia upanga wake
9. Amri ya Mungu ilisema kwamba Sanduku hilo halikupasa kuguswa kamwe na watu ambao hawakuwa wameruhusiwa
10. Apolonia
11. ‘Kutoka macheo ya jua’
12. 40
13. Penye bubujiko la Yakobo
14. ‘Zitaendelea kwenye ukosefu wa kumwogopa Mungu zaidi na zaidi’
15. Shemu, Hamu, na Yafethi
16. Ezeri
17. “Bila shaka, roho ni yenye hamu, lakini mwili ni dhaifu”
18. Daudi
19. Maria Magdalene, Salome, Yoana, na Maria mama ya Yakobo