Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon

Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon

Nzumari za Nyasi za Visiwa vya Solomon

Na mwandishi wa Amkeni! katika Visiwa vya Solomon

JE, UMEWAHI kujaribu kupiga nzumari? Unapovuta na kutoa pumzi inavyotakikana unaweza kushikwa na kizunguzungu. Lakini ebu wazia kupiga nzumari zenye urefu wa meta mbili na kipenyo cha sentimeta tano, huku ukisogeza mwili wako wote ili kutokeza muziki. Nzumari 40 za aina hiyo huunganishwa ili kutengeneza ala moja ya nzumari za nyasi za Visiwa vya Solomon. Ndiyo, kila nzumari katika ala hiyo imetengenezwa kwa nyasi! Nyasi tofauti-tofauti za misitu ya tropiki ya Visiwa vya Solomon, hutumiwa kutengeneza nzumari zenye sauti nyembamba kabisa hadi zile zenye sauti nzito kabisa.

Tutembelee ghala fulani huko Honiara, ambamo kikundi cha Narasirato Pipers hutengeneza ala zao na kufanya mazoezi kabla ya kufunga safari ya kwenda Taiwan ili kufanya maonyesho ya muziki huko. Ala fulani zina nzumari tatu zilizounganishwa, nazo hutokeza noti tatu zilizolinganishwa. Wanamuziki wanashika nzumari hizo tatu pamoja na kuzigonga kwenye jiwe tambarare ili kuhakikisha zinatokeza noti zinazolingana. Zisipolingana, wanakata sehemu ya mwishomwisho ya nzumari isiyo na noti sawa. Nzumari hizo tatu zilizounganishwa hazipulizwi. Kipande cha mpira hufungwa kwenye sehemu ya chini ya kila nzumari. Muziki hutokezwa wakati nzumari zote zilizounganishwa zinapogongwa ardhini. Ni sauti ya ajabu iliyoje! *

Ni vigumu kueleza muziki unaotokezwa na nzumari hizo. Nyakati nyingine zinatokeza sauti nyororo sana; na nyakati nyingine mshindo mkubwa sana. Wanamuziki wanapopiga ala hizo wanabadilishana mahali pa kusimama kulingana na mpangilio maalumu. Nyakati nyingine muziki huo unatia hofu, lakini kwa kawaida hufurahisha. Huenda utaweza kututembelea siku moja na kusikia nzumari za ajabu za nyasi za Visiwa vya Solomon!

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 4 Nzumari nyingine hutokeza muziki zinapogongwa na kipande kinene cha mpira.