Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 24. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Kulingana na Yakobo, ni mambo gani yanayomtambulisha Mkristo wa kweli? (Yakobo 1:27)
2. Ni pigo gani la mwisho lililowakumba Wamisri na kuwafanya wawaachilie Waisraeli? (Kutoka 11:1, 5)
3. Ni herufi zipi katika alfabeti ya Kigiriki zinazotumiwa kumrejezea Yehova? (Ufunuo 1:8)
4. Kwa nini Yehova hakuwafukuza mara moja wakazi wa Bara Lililoahidiwa kutoka mbele ya Waisraeli? (Kutoka 23:29, 30)
5. Ni mambo gani matatu ambayo Rahabu alipaswa kufanya, ili kujiokoa na kuokoa familia yake? (Yoshua 2:18-20)
6. Shetani alimpiga Ayubu kwa ugonjwa upi? (Ayubu 2:7, 8)
7. Kwa nini Zakayo alipanda mti wa mforsadi-tini? (Luka 19:3, 4)
8. Daudi alikuwa na kaka wangapi? (1 Mambo ya Nyakati 2:15)
9. Malkia wa Sheba alijaribu hekima ya Solomoni jinsi gani? (1 Wafalme 10:1)
10. Ni neno lipi la Kiebrania linalowakilisha neno “Bwana”? (Mwanzo 15:2)
11. Wanafunzi wa Yesu waliokuwa Yudea wangeona nini na kukimbilia milimani? (Marko 13:14)
12. Kwa nini tuna tumaini hakika la kupata uhai udumuo milele? (Tito 1:2)
13. Mtoto Musa aliwekwa kwenye kisafina kilichokuwa kimetengenezwa na nini? (Kutoka 2:3, Biblia Habari Njema)
14. Yesu alituma wanafunzi wangapi wamtangulie katika kampeni yake ya mwisho ya kuhubiri huko Yudea? (Luka 10:1)
15. Mafarisayo walikuwa na kusudi lipi walipomwuliza Yesu maswali? (Mathayo 22:15)
16. Ni nini hata kitakacholipata “jina la mtu mwovu”? (Mithali 10:7)
Majibu kwa Maswali
1. “Kufuliza kujitunza mwenyewe bila doa kutokana na ulimwengu” na kuwajali mayatima au wajane
2. Kifo cha wazaliwa wote wa kwanza, tangu wanadamu hata wanyama
3. Alfa na omega
4. Ili kuzuia kuongezeka kwa wanyama wa pori katika bara lililoachwa ukiwa kwa ghafula
5. Kukusanya familia yake nyumbani mwake, kufunga kamba nyekundu dirishani, na kutosema lolote kuhusu ziara ya wapelelezi hao
6. Majipu mabaya tangu utosi wa kichwa hata wayo wa mguu
7. Hakuweza kumwona Yesu kwa sababu alikuwa mdogo kwa kimo
8. Sita
9. Alimwuliza “maswali ya fumbo”
10. Adonay [au Adhonai]
11. “Kile kitu chenye kuchukiza sana ambacho husababisha ukiwa kikiwa kimesimama ambapo hakipaswi”
12. Kwa sababu Mungu aliuahidi, na hawezi kusema uwongo
13. Mafunjo
14. 70 (vikundi 35 vya wawili-wawili)
15. ‘Kumtega katika usemi wake’
16. “Litaoza” na kutoweka