Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Kwa nini Isaya anasema kwamba miungu ya dhahabu na fedha itatupwa kwa popo katika siku ya Yehova? (Isaya 2:20)
2. Kwa nini Waisraeli waliambiwa wasivune kabisa kabisa pembe za mashamba yao? (Mambo ya Walawi 19:9)
3. Chini ya Sheria ya Musa, mtu aliyeharibu jicho au kung’oa jino la mtumwa wake alihitaji kufanya nini? (Kutoka 21:26, 27)
4. Mtu aliyemwua mwenzake pasipo kukusudia angekaa kwenye jiji la makimbilio hata lini? (Hesabu 35:25)
5. Ni muda gani ulipita tangu Kornelio aliposali kwa Mungu hadi Petro alipokuja kumwona? (Matendo 10:30-33)
6. Ni hatua gani ambayo Paulo anasema inapaswa kuchukuliwa kwa “wale wasababishao migawanyiko na sababu za kukwaza”? (Waroma 16:17)
7. Shetani alimsababishia Ayubu madhara gani ya afya alipojaribu kumfanya akane uaminifu wake? (Ayubu 2:7)
8. Waisraeli walikuwa wapi wakati sheria ya Sabato ilipoanza kutenda na walipokula mana kwa mara ya kwanza? (Kutoka 16:1)
9. Ehudi alitumia nini kumuua Mfalme Egloni wa Moabu? (Waamuzi 3:16)
10. Makutaniko saba ambayo Yohana alitumia ujumbe yalikuwa katika mkoa gani wa Roma? (Ufunuo 1:4)
11. Yesu anahusianishwa mara nyingi na mnyama gani, na kwa nini? (Yohana 1:29)
12. Ni neno lipi hutumiwa kutaja mkusanyo wa maji ili kuyatofautisha na nchi kavu? (Habakuki 2:14)
13. Noa alitumia nini kisichopenyeza maji katika ujenzi wa Safina? (Mwanzo 6:14)
14. Ni nini kilichotokea mbinguni baada ya Kristo kutawazwa? (Ufunuo 12:7)
15. Yesu alituma wanafunzi gani wawili wakatayarishe mwadhimisho wake wa mwisho wa Sikukuu ya Kupitwa? (Luka 22:7-13)
16. Ilikuwa imetabiriwa kuwa Yesu angepanda juu ya mnyama gani ili kuingia Yerusalemu kwa utukufu? (Zekaria 9:9)
17. Wavivu wanahimizwa kuiga njia za mdudu yupi? (Mithali 6:6)
18. Matokeo yalikuwa nini Petro alipotumia upanga wake akijaribu kumkinga Yesu? (Yohana 18:10)
19. Ni mdudu yupi ambaye Mafarisayo walijaribu kumchuja kwa uangalifu sana ili wasiwe najisi kisherehe? (Mathayo 23:24)
20. Ni nani anakumbukwa kwa kuwaheshimu wanawe kuliko Yehova? (1 Samweli 2:22, 29)
Majibu ya Maswali
1. Kwa sababu mahali pa giza na uchafu ndipo tu panapozifaa sanamu hizo bali si mahali penye heshima na umaarufu
2. Ili wanaoteseka na wageni wapate kitu cha kukusanya
3. Kumwacha huru yule mtumwa
4. Hadi kifo cha kuhani wa cheo cha juu
5. Siku nne
6. Kufuliza kuwaangalia na kuwaepuka
7. Alimpiga Ayubu kwa majipu mabaya yaliyojaa mwili mzima
8. Katika bara ya Sini
9. Upanga uliokuwa na makali kuwili
10. Asia
11. Mwana-kondoo.Kwa sababu ya fungu lake akiwa dhabihu
12. Bahari
13. Lami
14. Vita iliyosababisha kuvurumishwa kwa Shetani kutoka mbinguni
15. Petro na Yohana
16. Punda
17. Chungu
18. Alikatilia mbali sikio la kuume la Malko, mtumwa wa kuhani wa cheo cha juu
19. Inzi
20. Kuhani wa cheo cha juu Eli