Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

“Mwangaza Kamili”

“Mwangaza Kamili”

“Mwangaza Kamili”

IWAPO umewahi kugusa balbu ya taa ya umeme ambayo imewaka kwa muda fulani, unafahamu kwamba inakuwa moto sana. Joto hilo husababishwa na nishati inayopotea bure. Balbu ya kawaida hutumia asilimia 10 tu ya nishati yake kutoa mwangaza, na asilimia 90 iliyosalia hupotea bure na kubadilika kuwa joto. Kwa upande mwingine, yule mdudu mdogo anayeitwa kimulimuli, ambaye hutoa mwangaza, (ona juu, picha kubwa) hutumia karibu asilimia 100 ya nishati kutoa mwangaza.

Vimulimuli hupoteza nishati kidogo sana ambayo hubadilika kuwa joto. Ndiyo sababu mwangaza wao umeitwa “mwangaza kamili.” Wao hufanyaje hivyo? Tumbo la kimulimuli lina kitu kinachoitwa luciferin. Oksijeni inapoingia tumboni kupitia mrija fulani, inachanganyika na luciferin na kusababisha utendaji wa kemikali ambao hutoa mwangaza wenye rangi hafifu ya manjano na rangi nyekundu ya kijani.

Chembe zinazotoa mwangaza huo zina fuwele za asidi ya yurea. Fuwele hizo huelekeza mwangaza huo kutoka kwenye tumbo la kimulimuli. Wanasayansi wanasema kwamba vimulimuli huvutia wapenzi kwa mwangaza wao na kwamba aina mbalimbali za vimulimuli hutoa mwangaza kwa njia tofauti-tofauti.

Je, hukubali kwamba maumbile ya wadudu hao wadogo humsifu Muumba wao, Yehova Mungu? Naam, kama vile mtunga-zaburi alivyotangaza, “kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.”—Zaburi 150:6.

[Picha katika ukurasa wa 31]

© Darwin Dale/Photo Researchers, Inc.