Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Katika ndoto ya Mfalme Nebukadneza, malaika alisema mti mkubwa sana uliokatwa ungepewa nini, na hiyo ilimaanisha nini? (Danieli 4:16)

2. Samsoni aliwasimulia Wafilisti nini wakati wa karamu yake ya arusi ambacho kiliongoza kwenye tukio ambapo aliwaua Wafilisti 30 huko Ashkeloni? (Waamuzi 14:12-19)

3. Ni mfalme yupi wa Babiloni aliyelazimika kuamuru Danieli atupwe katika tundu la simba, kwa sababu ya sheria isiyoweza kubadilika? (Danieli 6:9)

4. Mfalme Ahasuero aliwatuma wasimamizi wangapi wa nyumba wampeleke Malkia Vashti mbele yake ili awaonyeshe watu urembo wake? (Esta 1:10)

5. Kulingana na Yakobo, ni mambo gani mawili ambayo Mungu anataka katika “ibada iliyo safi na isiyo na unajisi?” (Yakobo 1:27)

6. Iwapo mtumwa Mwebrania hakutaka kuwekwa huru na bwana wake, bwana huyo alipaswa kufanya nini? (Kutoka 21:6)

7. Ni wana gani wawili wa Eliabu Mreubeni waliounga mkono uasi wa Kora dhidi ya Musa na Aroni? (Hesabu 16:1-3)

8. Waisraeli hawakupaswa kuumbua ngozi yao kwa njia gani? (Mambo ya Walawi 19:28)

9. Ni nani aliyekuwa mama ya Mfalme Hezekia? (2 Wafalme 18:2; 2 Mambo ya Nyakati 29:1)

10. Kulingana na Solomoni, “kila kusudi chini ya mbingu” lina nini? (Mhubiri 3:1)

11. Yehova alimwamuru Yeremia afanye nini wakati Mfalme Yehoyakimu alipoteketeza hati ya kukunja baada ya kusikia baadhi ya mashutumu yaliyokuwamo? (Yeremia 36:27-32)

12. Ni nani aliyejulikana kuwa kuhani na mwandishi stadi? (Nehemia 8:9)

13. Kwa nini wana wa Yakobo hawakukubali ombi la baba yao la kurudi Misri kununua chakula zaidi wakati kulipokuwa na njaa? (Mwanzo 43:1-5)

14. Ni katika njia gani Adamu aliumbwa “kwa sura ya Mungu”? (Mwanzo 5:1)

15. Ni mmea upi wenye harufu kali sana ambao Yesu alitaja wakati aliposema kuhusu Mafarisayo washupavu waliotoa sehemu ya kumi na kupuuza “mambo yenye uzito zaidi ya Sheria”? (Mathayo 23:23)

16. Yeremia alitahini utii wa Warekabi kwa njia gani? (Yeremia 35:3-6)

17. Ndugu kumi za Yosefu walimdanganyaje baba yao ili aamini kwamba Yakobo alikuwa ameuawa na mnyama-mwitu? (Mwanzo 37:31-33)

18. Ingawa huenda mengine yalikuwa makubwa zaidi, ni jitu gani maarufu ambalo limetajwa katika Biblia? (1 Samweli 17:4)

19. Musa alikufa juu ya mlima gani, baada ya kulitazama Bara Lililoahidiwa? (Kumbukumbu la Torati 32:49, 50)

20. Tabenakulo na mahekalu ya baadaye yalijengwa kwa kuelekea upande gani? (Hesabu 3:38)

Majibu ya Maswali

1. “Moyo wa mnyama.” Kwamba Nebukadneza angepoteza fahamu na kuwa kama mnyama

2. Kitendawili

3. Dario

4. Saba

5. “Kutazama mayatima na wajane katika dhiki yao, na kufuliza kujitunza mwenyewe bila doa kutokana na ulimwengu”

6. Kumleta mbele ya mlango au penye mwimo wa mlango na ‘kutoboa sikio lake kwa uma’

7. Dathani na Abiramu

8. Kuchora alama mwilini mwao

9. Abiya

10. “Majira yake”

11. Aandike hati nyingine ndefu zaidi

12. Ezra

13. Mtawala wa Misri aliwaambia kwamba hawakupaswa kurudi bila ndugu yao mdogo, Benyamini

14. Alikuwa na akili na uwezo mwingi zaidi kuliko viumbe wengine wote duniani, kama vile sifa za kiroho na maadili

15. Mnanaa

16. Aliwawekea divai waliyokuwa wamekatazwa na babu yao wa kale, na kuwaambia wainywe

17. Waliichovya kanzu ndefu ya Yosefu katika damu ya mbuzi na kumwonyesha Yakobo

18. Goliathi

19. Nebo

20. Mashariki