Jukumu la Vyombo vya Habari
Jukumu la Vyombo vya Habari
“Wakati mmoja Mwanzilishi wa makampuni ya magazeti ya Scripps, Edward Willis Scripps, alisema kwamba jukumu la vyombo vya habari nchini Marekani ni kuwastarehesha watu wanaotaabishwa na kuwataabisha wale ambao wamestarehe,” ndivyo alivyosema Mike McCurry, aliyekuwa msimamizi wa habari katika ikulu ya White House. Aliongeza hivi: “Huwezi kuwastarehesha au kuwataabisha watu bila kuwapa habari kwanza.”
“[McCurry] alisema kwamba njia zetu za kufahamu matukio ya ulimwengu zina kasoro kwa sababu vyombo vyetu vya habari [vya Marekani] haviripoti yale yanayoendelea ulimwenguni.” Kwa kusikitisha, vyombo vya habari vya Marekani vinaamini kwamba “Wamarekani hawapendi kujua mambo yanayoendelea ulimwenguni.”—Graphic Arts Monthly.
Gazeti la Amkeni! lina waandishi katika sehemu zote za ulimwengu na lengo lake ni kuwafahamisha wasomaji kuhusu matukio ya karibuni, habari za kisayansi na za kijamii. Gazeti hilo huimarisha uhakika katika Muumba mwenye upendo. Hilo huchapishwa katika lugha 87, na 61 kati ya hizo hutolewa kwa wakati mmoja. Zaidi ya nakala milioni 21 huchapishwa katika kila toleo! Amkeni kwa kusoma Amkeni!
[Picha katika ukurasa wa 31]
Utumwa wa Aina Zote Utakapokoma!
[Picha katika ukurasa wa 31]
Je, Inawezekana Kupatanisha Sayansi na Dini?
[Picha katika ukurasa wa 31]
Je, Kucheza Kamari Ni Tafrija Isiyodhuru?
[Picha katika ukurasa wa 31]
Msaada kwa Wanawake Wanaopigwa
[Picha katika ukurasa wa 31]
Je, Amani ya Ulimwenguni Pote Ni Ndoto Tu?