Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Jinsi Mambo Yalivyoanza

Jinsi Mambo Yalivyoanza

Jinsi Mambo Yalivyoanza

JAMII ndogo ya watu inaishi katika eneo la Stratton huko Ohio, Marekani, karibu na Mto Ohio. Mto huo unapita kati ya jimbo la Ohio na jimbo la West Virginia. Stratton ni kijiji ambacho kina meya. Mnamo mwaka 1999, mgogoro ulizuka katika jamii hiyo ndogo yenye wakazi wasiofika 300 wakati wenye mamlaka wa eneo hilo walipojaribu kuwashurutisha Mashahidi wa Yehova, na wengine, kupata kibali kabla ya kuwatembelea watu nyumbani kwao kuwaeleza ujumbe wa Biblia.

Kwa nini hilo ni jambo zito? Unapoendelea kusoma simulizi hili, utaona kwamba amri hiyo ya wenye mamlaka haingedhibiti tu haki ya uhuru wa kusema ya Mashahidi wa Yehova bali pia ya watu wote wanaoishi Marekani.

Jinsi Mgogoro Huo Ulivyoanza

Wahudumu wa Kutaniko la Mashahidi wa Yehova la Wellsville lililo karibu walikuwa wamewatembelea wakazi wa Stratton kwa miaka mingi. Tangu mwaka 1979, wahudumu hao walikuwa wametatizwa na maafisa kadhaa wa eneo hilo kuhusu kazi yao ya kuhubiri nyumba hadi nyumba. Mapema katika miaka ya 1990, polisi mmoja wa eneo hilo alifukuza kikundi cha Mashahidi mjini, akisema: “Mimi sijali haki zenu.”

Mambo yalichacha mnamo mwaka 1998 wakati meya wa Stratton alipowakabili Mashahidi wanne wa Yehova ana kwa ana. Walikuwa wakitoka kwenye kijiji hicho kwa gari baada ya kuwatembelea tena wakazi waliopendezwa na mazungumzo ya Biblia. Kulingana na mmoja wa wanawake waliokabiliwa, meya alisema kwamba kama wangekuwa wanaume, angewafunga gerezani.

Mgogoro wa hivi majuzi ulisababishwa na amri ya wenye mamlaka wa kijiji hicho ambayo “Ilikataza Kuuza na Kuombaomba Kwenye Makao ya Watu Bila Ruhusa.” Amri hiyo ilisema kwamba watu wanaotaka kwenda nyumba hadi nyumba kufanya shughuli mbalimbali wanapaswa kupata kibali kutoka kwa meya bila malipo. Mashahidi wa Yehova walionelea kwamba amri hiyo inaingilia uhuru wa kusema, uhuru wa dini, na uhuru wa kusambaza habari. Basi, wakawasilisha kesi mbele ya mahakama ya serikali kwa kuwa wenye mamlaka wa kijiji hicho walikataa kubatilisha amri hiyo.

Mnamo Julai 27, 1999, kesi hiyo ilisikilizwa na jaji wa mahakama moja ya wilaya katika Wilaya ya Kusini ya Ohio. Jaji huyo aliamua kwamba amri hiyo ya kuomba kibali ni halali. Baadaye, mnamo Februari 20, 2001, Mahakama ya Rufaa ya Marekani ya Eneo la Sita iliamua tena kwamba amri hiyo inapatana na katiba.

Ili mgogoro huo utatuliwe, shirika la Watchtower Bible and Tract Society of New York na Kutaniko la Mashahidi wa Yehova la Wellsville liliomba Mahakama ya Juu ya Marekani isikilize tena kesi hiyo.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 3]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Los Angeles

New York

OHIO

Stratton