Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuzoea Simu za Mkononi “Kupita Kiasi”

Kuzoea Simu za Mkononi “Kupita Kiasi”

Kuzoea Simu za Mkononi “Kupita Kiasi”

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI JAPAN

GAZETI The Daily Yomiuri la Japan lilikuwa na kichwa cha habari: “Wamezoea Simu za Mkononi Kupita Kiasi.” Kupita kiasi? Gazeti hilo lilieleza: “Ni kama vijana wanaona simu za mkononi zikiwa sehemu ya mwili wao na hata huwa na wasiwasi wasipokuwa nazo.” Wakiogopa kukatiza mawasiliano na wenzao, vijana wengi hawazimi kamwe simu zao za mkononi wakati wowote, mahali popote. “Wanapokosa kupokea ujumbe wowote kupitia simu, wao huwa na wasiwasi na huudhika, na kuanza kuhisi hawapendwi na mtu yeyote.” Wasiwasi huo huwafanya wajibu mara moja ujumbe wowote wa maandishi wanaopokea, jambo ambalo si la lazima.

Pasipo shaka, simu za mkononi zina manufaa. Kwa hakika, zimetumiwa katika hali za dharura. Hata utumizi wa simu za mkononi katika hali nyingine si mbaya, maadamu zinatumiwa kwa usawaziko. Hata hivyo, wataalamu fulani husema kwamba utumizi wa “kupita kiasi’ wa simu hizo unaweza kuzuia mawasiliano ya kawaida. Mwalimu mmoja wa shule ya upili huko Osaka anahofia kwamba simu za mkononi zinawafanya “watoto washindwe kuelewa ishara za uso, tabia na hali za sauti za watu wengine. Kwa sababu hiyo, jeuri imeongezeka baina ya watoto na hawazingatii hisia za watu wengine,” likasema gazeti hilo.

Makala hiyo ilimalizia kusema: “Inaonekana kwa hakika kwamba watoto wataendelea kuzoea simu za mkononi zaidi wakati ujao. Njia pekee ya kupunguza kuongezeka kwa tatizo hilo ni wazazi kuhakikisha kwamba wamewawekea watoto wao mfano mzuri katika utumizi wa simu za mkononi.”