Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 13. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Musa na Haruni walikuwa wapi walipokosa kumtakasa Yehova, hivyo wakapoteza pendeleo la kuingia katika Nchi ya Ahadi? (Hesabu 20:12, 13)

2. Ni genge gani la wavamizi lililoiba ng’ombe na punda wa Ayubu na kuwaua watumishi wake? (Ayubu 1:14, 15)

3. Kati ya waandamani watatu wa Danieli, ni nani aliyeitwa Meshaki walipokuwa Babiloni? (Danieli 1:7)

4. Ni tunda gani la roho ambalo limetajwa baada ya upendo? (Wagalatia 5:22)

5. Malaika mwenye nguvu alilivurumisha wapi “jiwe kama jiwe kubwa la kusagia” ili kuonyesha uharibifu wa ghafula wa Babiloni Mkubwa? (Ufunuo 18:21)

6. Gehazi alimwomba Naamani zawadi zipi akitumia jina la Elisha kwa uwongo? (2 Wafalme 5:22)

7. Ni mfalme yupi Mwamori aliyewazuia Waisraeli wasipite katika ufalme wake, ingawa Waisraeli waliahidi hata hawangekunywa maji huko? (Hesabu 21:21-23)

8. Ni nani aliyemuuzia Abrahamu pango la Makpela ili amzike Sara humo? (Mwanzo 23:8-10)

9. Kulingana na Mithali 29:25, “kuwaogopa wanadamu” hutokeza tatizo gani, na kunaweza kuepukwaje?

10. Ni tunda gani la roho ya Mungu linaloorodheshwa katika nafasi ya tatu? (Wagalatia 5:22)

11. Finehasi alichukua hatua gani iliyomfurahisha Yehova na kumfanya akomeshe pigo lililowaua Waisraeli 24,000? (Hesabu 25:6-14)

12. Bathi, kibaba, kori, efa, hini, homeri, logi, na omeri vilikuwa nini? (Kutoka 16:32)

13. Mitume na wanaume wazee wa Yerusalemu waliorodhesha ‘mambo gani ya lazima’ walipowaandikia akina ndugu huko Antiokia, Siria, na Kilikia? (Matendo 15:28, 29)

14. Kwa nini malkia wa Sheba alisafiri mbali sana hadi Yerusalemu? (1 Wafalme 10:4)

15. Ni jambo gani la pekee lililopasa kuzingatiwa katika kila kusanyiko takatifu ambalo Yehova aliwaagiza Waisraeli wafanye? (Mambo ya Walawi 23:7)

16. Ni kitabu gani kifupi zaidi kati ya vitabu vinne vya Injili?

17. Ni nani aliyepigwa kwa upanga na Petro na sikio lake la kuume kukatiliwa mbali, wakati umati ulipokuja kumkamata Yesu? (Yohana 18:10)

18. Biblia iliandikwa kwa lugha gani tatu hapo awali? (Ezra 4:7; Ufunuo 9:11)

19. Ni watu gani waliojulikana kuwa wahamaji, wakiishi kwenye mahema na kufuga wanyama? (Yeremia 3:2)

20. Kwa nini Waisraeli hawakupaswa kuvuna pembe za mashamba yao kabisa-kabisa? (Mambo ya Walawi 19:9, 10)

Majibu kwa Maswali

1. Kwenye maji ya Meriba

2. Waseba

3. Mishaeli

4. Shangwe

5. Baharini

6. “Talanta ya fedha, na mavazi mawili”

7. Sihoni

8. Efroni Mhiti

9. Huleta mtego. Kumtumaini Yehova

10. Amani

11. Alimwua Zimri mkuu wa kabila la Simeoni na mwanamke Mmidiani ambaye Zimri alimleta kwenye hema lake ili afanye uasherati naye

12. Vipimo

13. “Kuendelea kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu na damu na kutokana na vitu vilivyonyongwa na uasherati”

14. ‘Kuona hekima yote ya Sulemani’

15. Hawakupaswa kufanya kazi yoyote ngumu

16. Marko

17. Malko, mtumwa wa kuhani wa cheo cha juu

18. Kiebrania, Kiaramu, na Kigiriki

19. Waarabu

20. Ili waache kiasi fulani cha nafaka “kwa ajili ya maskini na mgeni”