Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 20. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Samsoni alimchagua nani awe mke wake wakati ‘alipotaka kisa juu ya Wafilisti’? (Waamuzi 14:1-4)

2. Yesu alisema kwamba ikiwa mtu ni mtumwa wa Mungu, hawezi kuwa mtumwa wa nini? (Luka 16:13)

3. Ni babu yupi wa kale wa Mesiya aliyekuwa mume wa Ruthu? (Ruthu 4:13)

4. Wasomi wengi wa Kiebrania wanapendelea kutamka jina la Mungu vipi?

5. Yehova alitabiri kwamba Yezebeli angepatwa na nini kwa sababu ya uovu wake mwingi? (1 Wafalme 21:23)

6. Kwa nini Abrahamu alinunua pango la Makpela kutoka kwa “wazawa wa Hethi”? (Mwanzo 23:19, 20)

7. Ni usemi upi ambao hapo awali ulimaanisha kuunganisha pindo za nguo ili kujitayarisha kufanya kazi, umetumiwa katika Maandiko kuonyesha kujitayarisha kwa ajili ya shughuli ya kiakili au ya kiroho inayohitaji jitihada nyingi? (Ayubu 38:3)

8. Ni mwana yupi wa Adamu na Hawa aliyezaliwa wakati Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130? (Mwanzo 5:3)

9. Waisraeli walishindwa huko Ai kwa sababu ya dhambi ya nani? (Yoshua 7:20)

10. Kwa kuwa Maria hangeweza kutoa dhabihu ya kondoo-dume wakati Yesu alipozaliwa, Sheria ilimruhusu kutoa dhabihu gani nyingine? (Luka 2:24)

11. Paulo alijitambulishaje katika barua zake nyingi zilizoongozwa na roho ya Mungu? (Waefeso 1:1)

12. Wakati ambapo Mfalme Senakeribu Mwashuri alipokuwa akijaribu kuwafanya Wayahudi wasalimu amri, kwa nini Hezekia alichukizwa hasa na dhihaka zake? (Isaya 36:14, 15, 18-20)

13. Paulo alikuwa wapi alipopata mwito huu: “Vuka uingie Makedonia utusaidie”? (Matendo 16:8, 9)

14. Kwa nini Hanani yule mwonaji alimkemea Mfalme Asa wa Yuda aliyekuwa mwema baada ya kutawala kwa uaminifu kwa miaka mingi? (2 Mambo ya Nyakati 16:7)

15. Yesu alisema kwamba mtu anapaswa kuvumilia kwa uaminifu kwa muda gani ili aokolewe? (Marko 13:13)

Majibu kwa Maswali

1. Mwanamke Mfilisti wa Timna

2. Mali

3. Boazi

4. Yahweh

5. ‘Mbwa wangemla Yezebeli’

6. Ili amzike Sara mke wake humo

7. “Jifunge viuno”

8. Sethi

9. Akani

10. “Jozi moja ya njiwa-tetere au hua wachanga wawili”

11. Kama mtume wa Kristo Yesu

12. Kwa sababu Senakeribu alijisifu kwa kusema kwamba Yehova hana uwezo, kama ile miungu ya mataifa yaliyokuwa yameshindwa

13. Huko Troasi, bandari iliyoko Asia Ndogo

14. Kwa kuwa wakati huo Mfalme Asa alikuwa ameungana na mfalme wa Siria badala ya kumtegemea Yehova kwa sababu isiyojulikana

15. “Hadi mwisho”