Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Koreshi, Dario, Ahasuero, na Artashasta walitawala ufalme gani? (Ezra 4:5-7)

2. Yakobo aliufananisha ulimi na nini alipoonyesha nguvu ya ulimi katika kuuelekeza mwili mzima? (Yakobo 3:3, 4)

3. Ni nani anayetajwa kuwa wa kwanza kutumia jina la Mungu? (Mwanzo 4:1)

4. Majina ya wale ambao wamethibitika kuwa waaminifu kwa Yehova yameandikwa wapi? (Ufunuo 20:12)

5. Maelezo kuhusu Leviathani katika kitabu cha Ayubu 41:1-34 yanafaa mnyama yupi hasa?

6. Malkia Vashti alikataa kufanya nini kilichomkasirisha Mfalme Ahasuero na kumfanya amwachishe kuwa malkia? (Esta 1:12, 19)

7. Ni nani walioleta ripoti nzuri kati ya wale watu 12 waliotumwa na Musa kupeleleza nchi ya Kanaani? (Hesabu 14:6-8)

8. Shetani atafungwa katika abiso kwa muda gani? (Ufunuo 20:1-3)

9. Eliya alitumia nini kumweka Elisha kuwa nabii badala yake? (1 Wafalme 19:16, 19)

10. Yehova alionyeshaje kwamba Haruni na nyumba yake walikuwa wamechaguliwa kuwa makuhani wakati mamlaka ya Musa na Haruni yalipopingwa? (Hesabu 17:1-11)

11. Mwanzoni Sauli alimwahidi Daudi kwamba angempatia nani awe mkewe? (1 Samweli 18:17-19)

12. Ni jibu la aina gani ambalo “hugeuza hasira”? (Mithali 15:1)

13. Kama Yesu alivyotaja, ni nani aliyesema kwamba mtu na mkewe “watakuwa mwili mmoja”? (Mathayo 19:4-6)

14. Wayahudi walipomshtaki Paulo kuwa anawashawishi watu wamwabudu Mungu kwa njia tofauti, ni nani aliyeipuuza kesi hiyo kwa sababu Paulo hakuwa amevunja sheria ya Roma? (Matendo 18:12-16)

15. Katika kielezi cha Yesu kuhusu kabaila aliyeondoka nyumbani “ili ajipatie mamlaka ya kifalme,” watumwa walipewa nini? (Luka 19:12-24)

16. Sulemani alimaliza kujenga hekalu huko Yerusalemu katika mwezi gani? (1 Wafalme 6:38)

Majibu ya Maswali

1. Uajemi

2. Mtambo mdogo wa usukani wa meli kubwa

3. Hawa

4. Katika “hati-kunjo ya uhai”

5. Mamba

6. Alikataa kufika mbele ya mfalme

7. Yoshua na Kalebu

8. Miaka 1,000

9. Vazi lake

10. Kati ya zile fimbo zote za wale viongozi wa makabila 12, fimbo ya Haruni tu ndiyo iliyochanua maua na kuzaa lozi mbivu

11. Binti yake mkubwa, Merabu

12. La upole

13. Mungu

14. Galio, prokonso wa Akaya

15. Mina

16. Buli, mwezi wa nane wa kalenda takatifu