Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Dawa ya Wadudu ya Nyani!

Dawa ya Wadudu ya Nyani!

Dawa ya Wadudu ya Nyani!

KATIKA misitu ya mvua ya Venezuela kuna nyani mwerevu sana, mwenye kichwa-kabari anayeitwa capuchin. Mvua inaponyesha katika makao ya nyani huyo, huleta mbu wengi wakali. Mbali na kuwa wasumbufu, wadudu hao wanaovamia ni hatari. Mara nyingi mbu hao hubeba mayai ya pange, ambayo yanapopachikwa ndani ya ngozi ya nyani, yanaweza kutokeza uvimbe hatari, ambao hutunga usaha.

Yamkini ili kujikinga kutokana na uvamizi huo, nyani hao hujipaka dawa kali ya asili kwenye miili yao—umajimaji unaotokana na aina fulani ya jongoo. Majongoo hao hutokeza michanganyiko miwili ya umajimaji ambayo huzuia kabisa wadudu. Umajimaji huo huwa na nguvu kuliko dawa za kufukuza wadudu zinazotengenezwa na mwanadamu ambazo hutumiwa na wanajeshi!

Kwa hiyo, wakati wa majira ya mvua, nyani huyo mwenye kichwa-kabari hugonga-gonga maganda ya miti au vichuguu akitafuta majongoo wenye urefu wa sentimeta 10. Anapompata mmoja, hujisugua kwa jongoo huyo mwili wake mzima—kutoka kichwani hadi mguuni. “Umajimaji huo hutafutwa sana na nyani hao hivi kwamba nyani wanne wanaweza kutumia jongoo mmoja,” lasema Journal of Chemical Ecology. Hata utaratibu ambao hufuatwa wakati wa kula na katika vipindi vingine, hutupiliwa mbali wakati nyani wanapopata jongoo wa kujipaka mwilini.

[Picha katika ukurasa wa 15]

Umajimaji wa jongoo

[Hisani]

Thomas Eisner/Cornell University

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 15]

Dr. Zoltan Takacs