Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Katika Biblia, ni wenzi gani waliokuwa wa kwanza kuzikwa katika pango la Makpela karibu na Hebroni, na ni nani wengine waliozikwa humo? (Mwanzo 49:29-33; 50:13)

2. Ni mwana yupi wa Daudi aliyejulikana kwa sura yake nzuri sana? (2 Samweli 14:25)

3. Paulo alikuwa raia wa nchi gani tangu kuzaliwa? (Matendo 22:25-28)

4. Adamu alipewa onyo gani kuhusu tunda lililokatazwa? (Mwanzo 2:17)

5. Baada ya Mfalme Rehoboamu kukataa shauri la watu, alimtuma nani kwa yale makabila ya kaskazini yaliyoasi, na mtu huyo alipatwa na nini? (2 Mambo ya Nyakati 10:18)

6. Yesu alimaanisha nini aliposema kwamba “hakuna awezaye kutumikia kama mtumwa mabwana-wakubwa wawili”? (Mathayo 6:24)

7. Yehova alipowapa Waisraeli mana, ile ambayo haikuokotwa ilienda wapi? (Kutoka 16:21)

8. Ni nani aliyemsaliti Yesu? (Luka 6:16)

9. Ni nani aliyekuwa mungu mkuu wa sanamu wa Waamoni? (Sefania 1:5)

10. Ni kiungo gani cha mwili kinachotumiwa mara nyingi katika Biblia kuwakilisha uwezo au nguvu nyingi? (Yeremia 32:17)

11. Ni nani aliyemwambia Mfalme Ahasuero kwamba Vashti anapaswa kuondolewa na mahali pake pachukuliwe na malkia mwingine? (Esta 1:14-20)

12. Musa alifanyaje maji machungu ya Mara yakawa matamu? (Kutoka 15:23-25)

13. Waisraeli walianzia wapi safari yao ya kutoka Misri? (Kutoka 12:37)

14. Ni nani aliyemfahamisha Yosia kuhusu maendeleo ya kazi ya kurekebisha hekalu na kumsomea mfalme huyo kile “kitabu cha torati” kilichopatikana humo? (2 Wafalme 22:8-10)

15. Kulingana na Ufunuo, farasi wanne ambao Yohana aliona walikuwa wa rangi zipi, na walifananisha nini? (Ufunuo 6:2-8)

Majibu ya Maswali

1. Abrahamu na Sara; pia Isaka, Rebeka, Lea, na Yakobo

2. Absalomu

3. Roma

4. “Siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”

5. Adoramu, msimamizi wa shokoa. Alipigwa mawe hadi akafa

6. “Hamwezi kutumikia kama watumwa Mungu na Utajiri”

7. ‘Jua lilipokuwa kali, iliyeyuka’

8. Yudasi Iskariote

9. Malkamu

10. Mkono

11. Memukani, msemaji wa wale maakida saba wa Umedi na Uajemi

12. ‘BWANA alimwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji’

13. Ramesesi

14. Shafani, mwandishi wa mfalme

15. Nyeupe—vita vya uadilifu; rangi-moto—vita vya wanadamu; nyeusi—njaa; kijivujivu—kifo