Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Utapiamlo Nilisoma kwa makini sana mfululizo “Utapiamlo—‘Hatari Iliyofichika.’” (Februari 22, 2003) Huku Japan hatuna tatizo hilo sana, kwa hiyo mambo niliyosoma yalinishangaza sana. Natumaini habari njema za Ufalme wa Mungu zitahubiriwa zaidi kwa watu wote wanaokumbwa na tatizo hilo.

Y. T., Japan

Video za Muziki Nyakati nyingine mimi hupokea magazeti yenu kutoka kwa rafiki yangu ambaye ni Shahidi wa Yehova. Nafikiri makala “Vijana Huuliza . . . Je, Inafaa Nitazame Video za Muziki?” (Februari 22, 2003) iliandikwa vizuri sana. Ilitaja mambo waziwazi na kuonyesha hatari za muziki wa kisasa.

M. M., Japan

Nilipopata gazeti hilo nilisoma makala hiyo mara moja. Rafiki zangu wengi hutazama video za muziki, na hupenda kuzungumza kuhusu video hizo. Makala hiyo imenisaidia nikinze kishawishi cha kuzitazama. Nina umri wa miaka 12, na makala hiyo ilikuja kwa wakati unaofaa kabisa.

K. W., Marekani

Niliifurahia sana makala hiyo. Mimi ni mhubiri wa wakati wote na ninajua kwamba ni muhimu niwe mfano bora kwa vijana wengine. Kwa hiyo nikiulizwa na vijana kwa nini sijatazama video fulani, nitasema kwamba sitaki kuharibu uhusiano wangu pamoja na Yehova. Tafadhali endeleeni kuchapisha makala zenye kuarifu za “Vijana Huuliza . . . ”

R. B., Marekani

Karibuni nitakuwa na umri wa miaka 21, nami hupenda kutazama video za muziki. Mlisema kweli kwamba video hizo huathiri wale wanaozitazama. Mara nyingi, vijana hupenda muziki kwa sababu ya mdundo lakini hawajali maneno yake, hasa muziki wa lugha ya kigeni. Mara nyingi video hizo huonyesha ujumbe wa muziki huo. Nyakati nyingine mimi hushangaa ninapotazama video ya muziki ambao nilidhani unafaa! Ninapoona video chafu, mimi hufungua kituo kingine na kuacha kabisa kusikiliza muziki huo.

T. G., Ufaransa

Nyumbu Nilifurahia sana makala yenye kichwa “Kundi Kubwa Lahama.” (Februari 22, 2003) Napenda wanyama. Gazeti jipya la Amkeni! linapofika, mimi huanza kusoma makala kuhusu wanyama. Nilishangaa kusoma kwamba nyumbu-jike anapokabili hatari anaweza kuacha kuzaa kisha akaendelea anapokuwa mahali salama! Tafadhali endeleeni kuchapisha makala kama hizo zenye kusisimua.

K. R., Italia

Dhambi Isiyosameheka Namshukuru sana Yehova na nyinyi pia kwa makala “Maoni ya Biblia: Je, Kuna Dhambi Isiyosameheka?” (Februari 8, 2003) Nimekuwa nikitafuta habari kama hiyo kwa muda fulani. Nilikuwa nikijaribu kuelewa andiko la Waebrania 10:26, na nilifikiri linawahusu tu wale 144,000, watakaoenda mbinguni. Asanteni kwa kufafanua jambo hilo.

R. A. P., Ghana

Siria Nilithamini sana uandishi wa pekee mliotumia katika makala “Historia Inayopendeza ya Siria.” (Februari 8, 2003) Kwa kuwa ninapenda sana historia na jiografia, nilifurahia kuhusianisha maandiko ya Biblia na mahali hususa kwenye ramani. Natumaini kwamba mtachapisha makala nyingine kama hiyo.

M. P., Ufaransa

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 30]

UN/DPI Photo by Eskinder Debebe