Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Sabuni Ni “Chanjo”

Sabuni Ni “Chanjo”

Sabuni Ni “Chanjo”

KISABABISHI cha pili kikuu cha vifo vya watoto duniani si malaria, wala kifua-kikuu, wala UKIMWI. Ni . . . ugonjwa wa kuharisha,” laripoti gazeti The Economist. Hata hivyo, watoto wengi wangekuwa hai leo iwapo wao na familia zao zingenawa mikono kwa sabuni kwa ukawaida.

Watafiti wa Taasisi ya London ya Usafi na Tiba ya Kitropiki waligundua kwamba “kunawa mikono vizuri kunaweza kupunguza magonjwa ya kuharisha kwa asilimia 43,” lasema gazeti The Economist. “Kunawa mikono kunaweza pia kupunguza magonjwa ya mfumo wa kupumua, ambayo ndiyo kisababishi kikuu cha vifo vya watoto. Uchunguzi mkubwa uliowahusu wanajeshi wa Marekani ulifunua kwamba mafua na kukohoa kulipungua kwa asilimia 45 wakati wanajeshi waliponawa mikono mara tano kwa siku.” Katika nchi zinazoendelea, familia nyingi zinaweza kununua sabuni. Hivyo, sabuni imetajwa kwa kufaa kuwa “chanjo ambayo mtu hujipatia” na haisababishi maumivu!

Biblia pia huwashauri watu wawe safi. Andiko la 2 Wakorintho 7:1 linasema: “Tujitakase na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu.” (Biblia Habari Njema) Ingawa Mungu anataka hasa tuwe safi kiroho, anaona usafi wa kimwili kuwa muhimu pia. (Mambo ya Walawi, sura ya 12-15) Bila shaka hatarajii tuwe safi kupita kiasi. Hata hivyo, tunapaswa kunawa mikono kwa ukawaida baada ya kutoka chooni, baada ya kumwosha au kumbadilisha mtoto napi, kabla ya kupika au kula, na wakati wowote ambapo kuna uwezekano wa kuwaambukiza wengine viini au virusi hatari. Kwa kunawa mikono kwa ukawaida, tunaonyesha upendo wa Kikristo kwa familia yetu na kwa wote tunaokutana nao.—Marko 12:31.