Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ngozi Yako Ni Kama “Ukuta wa Jiji”

Ngozi Yako Ni Kama “Ukuta wa Jiji”

Ngozi Yako Ni Kama “Ukuta wa Jiji”

Wakazi wa majiji ya zamani walijenga kuta ili kuzuia uvamizi. Ukuta wa jiji ulikuwa ngome ya kuzuia adui na kulinda jiji. Mwili wako vilevile una “ukuta”—ngozi yako. Ngozi yako hukulindaje?

Sehemu ya juu ya ngozi ina bakteria na vijiumbe vingine, na vingine vinaweza kusababisha maambukizo na magonjwa. Ngozi yako si kinga tu. Pia inatokeza protini zinazolinda mwili kwa kuua viini. Baadhi ya protini hizo hufanya kazi daima. Nyingine hutokea ngozi inapojeruhiwa.

Vikundi viwili vya protini za kuua viini ambavyo viligunduliwa kwanza, vinaitwa defensin na cathelicidin, na huwa tayari kulinda mwili nyakati zote. Vikundi vyote hivyo hutokezwa na chembe zilizo kwenye tabaka la juu la ngozi wakati ngozi inapojeruhiwa au kuvimba. Protini hizo huangamiza vijiumbe kwa kuvitoboa.

Katika mwaka wa 2001, kikundi cha watafiti wa Chuo Kikuu cha Tübingen, Ujerumani, kiligundua aina nyingine ya protini inayoangamiza viini inayoitwa dermicidin, ambayo hufanya kazi wakati wote. Tofauti na vile vikundi vingine viwili, dermicidin hutokezwa na tezi za jasho kwenye ngozi isiyojeruhiwa. Bado haijulikani jinsi protini hiyo hufanya kazi. Lakini kwa kuwa jasho husaidia kuzuia magonjwa, huenda hiyo ndiyo sababu watu wanaooga kupita kiasi hupata magonjwa ya ngozi na ukurutu.

Kama ukuta wa jiji la kale, ngozi yetu huzuia uvamizi wa adui. Ama kweli, utakubaliana na mtunga-zaburi aliyesema: “Jinsi kazi zako zilivyo nyingi, Ee Yehova! Zote umezifanya kwa hekima.”—Zaburi 104:24.