Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Vikalio vya msingi wa maskani vilitengenezwa na nini? (Kutoka 26:19-32)
2. Ukombozi wa taifa la Israeli kutoka utumwani Misri unaitwaje? (Waebrania 11:22)
3. Yesu alitabiri kwamba Petro angemkana mara ngapi? (Mathayo 26:75)
4. Kutaniko la Kikristo lilitambuliwa kwa sifa gani tatu baada ya zawadi za kimuujiza za roho kukoma? (1 Wakorintho 13:13)
5. Kwa nini kuabudu sanamu ni jambo la kipumbavu? (Zaburi 115:4-8)
6. Paulo aliwapa wanawake Wakristo shauri gani kuhusu mavazi? (1 Timotheo 2:9, 10)
7. Kwa nini Paulo alijiona kuwa “mdogo zaidi kati ya mitume”? (1 Wakorintho 15:9)
8. Samsoni alitumia silaha gani kuwaua wanaume 1,000 Wafilisti? (Waamuzi 15:15)
9. Ni mdudu gani ambaye ameliwa kwa karne nyingi huko Mashariki ya Kati? (Mambo ya Walawi 11:22)
10. Yohana Mbatizaji alitangaza nini kumhusu Yesu kwa siku mbili mfululizo? (Yohana 1:29, 35, 36)
11. Biblia hutumia viungo gani vilivyo ndani sana mwilini kuwakilisha hisia na fikira za ndani sana? (Ufunuo 2:23)
12. Katika ufunuo kwa Yohana, ni nani wanaoonekana wakiwa wameketi kuzunguka kiti cha ufalme cha Yehova? (Ufunuo 4:4)
13. Yesu alisema “mbegu ndogo zaidi kuliko zote duniani” ni gani? (Marko 4:31)
14. Paulo alipofika Athene katika safari yake ya pili ya umishonari, aliomba wanaume gani wawili “wamfuate upesi iwezekanavyo”? (Matendo 17:15)
15. Ni nani aliye Mpinzani mkuu wa Mungu? (Ayubu 1:6)
16. Ni nani aliyedhania kwamba Hana alikuwa mlevi na kumkemea? (1 Samweli 1:12-16)
17. Yule “mtu asiyefaa kitu” aliyemwasi Daudi na kuwafanya wanaume wote wa Israeli waasi, isipokuwa wale wa Yuda, alikuwa nani? (2 Samweli 20:1, 2)
18. Waisraeli walipokuwa nyikani walitamani vitu gani walivyokula huko Misri badala ya ile mana iliyoandaliwa kimuujiza? (Hesabu 11:5)
Majibu ya Maswali
1. Fedha
2. Kutoka
3. Tatu
4. Imani, tumaini, na upendo
5. Hazina uhai, zimetengenezwa na wanadamu
6. Kwamba yanapaswa kuwa yenye mpangilio mzuri na ya kiasi “kwa njia inayowafaa wanawake wanaodai kumheshimu Mungu”
7. Kwa sababu ‘alilitesa kutaniko la Mungu’
8. “Mfupa mbichi wa taya ya punda-dume”
9. Nzige
10. “Ona, Mwana-Kondoo wa Mungu!”
11. Figo
12. Yohana anaona wazee 24, wanaowakilisha wafuasi wa Yesu watiwa-mafuta wakiwa katika cheo chao huko mbinguni
13. “Mbegu ya haradali”
14. Sila na Timotheo
15. Shetani
16. Kuhani Mkuu Eli
17. Sheba
18. Samaki, matango, matikiti-maji, vitunguu vya majani, vitunguu, na vitunguu saumu