Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Michikichi Inayotegemezwa kwa Nguzo

Michikichi Inayotegemezwa kwa Nguzo

Michikichi Inayotegemezwa kwa Nguzo

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI PERU

MICHIKICHI ya aina hiyo hupatikana katika maeneo fulani ya ulimwengu. Lakini kwa nini michikichi itegemezwe kwa nguzo? Kwa sababu mzizi wa kwanza wa mchikichi huacha kukua unapofikia ukubwa fulani, lakini sehemu ile nyingine ya mchikichi huendelea kukua. Hivyo, shina hutokeza mizizi zaidi inayofanana na nguzo, na mizizi hiyo hushuka hadi ardhini.

Michikichi hiyo ina matumizi mengi. Wanyama wadogo huishi katikati ya mizizi ya miti hiyo. Mwanadamu pia hunufaika kutokana nayo. Katika nchi fulani, wenyeji hutumia mbao zake kujenga nyumba, kutia ndani sakafu, nao hutumia majani kuezeka paa, kutengeneza fagio, na kusuka vikapu. Huenda watu fulani wanaoishi mbali sana na misitu ya mvua ya tropiki wamewahi kutumia mikongojo maridadi au kukanyaga sakafu ngumu yenye kuvutia iliyotengenezwa kwa mbao za michikichi hiyo zenye rangi nyeusi ya kupendeza.

Kama michikichi mingi, michikichi hiyo huliwa. Sehemu ya katikati ya michikichi mingi ya aina hiyo huliwa na ina ladha tamu sana. Kwa kusikitisha, kwa kuwa watu wanazidi kupenda chakula hicho cha pekee, aina fulani za michikichi zimekatwa ili kupata tu sehemu yake laini ya katikati yenye ladha tamu, huku sehemu ile nyingine ya mti ikiachwa iharibike.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Michikichi hiyo hutumiwa kutengeneza bidhaa nyingi zenye faida