Je, Wajua?
Je, Wajua?
Maswali na Majibu
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Kulingana na Petro, kwa nini Mungu aliwafanya Waisraeli wa kiroho kuwa “jamii iliyochaguliwa”? (1 Petro 2:9)
2. Yesu alifanya muujiza gani kwanza, na aliufanya akiwa wapi? (Yohana 2:1-11)
3. Mungu alimfanya Hawa, mke wa Adamu, kutokana na nini? (Mwanzo 2:22)
4. Ni Mwisraeli gani mashuhuri aliyekuwa na wana “wasiofaa kitu”? (1 Samweli 2:12)
5. Ni kipimo gani katika nyakati za kale kilicholingana na homeri na bathi kumi? (Luka 16:7)
6. Ijapokuwa Mafarisayo walijua jinsi ya kufasiri kuonekana kwa anga, Yesu alisema hawawezi kufasiri nini? (Mathayo 16:3)
7. Katika unabii wa Ezekieli, ni nani watakaowashambulia watu wa Mungu wanaokaa kwa usalama na walio na ufanisi? (Ezekieli 38:14-16; 39:11)
8. Kwa nini Yesu alisema kwamba ibada ambayo viongozi wa kidini walitoa “kwa midomo yao” ilikuwa bure? (Marko 7:6, 7)
9. Ni mwana yupi wa Noa aliyefanya jambo lililosababisha mwana wake, Kanaani, alaaniwe? (Mwanzo 9:22-25)
10. Ni eneo la kabila gani ambalo baadaye liliwakilisha eneo la kaskazini kabisa mwa nchi ya Israeli? (Waamuzi 20:1)
11. Nyuzi ndefu katika chombo cha kufumia huitwaje? (Isaya 38:12)
12. Daudi alikubali kupewa adhabu gani kati ya zile adhabu tatu alizowekewa kwa kukosa kumtii Mungu na kuwahesabu Waisraeli? (2 Samweli 24:12-15)
13. Ezra, yule kuhani Myahudi aliandika vitabu gani vitatu vya Biblia?
14. Gavana Feliksi alihakikisha kwamba Paulo ametoka katika jimbo gani? (Matendo 23:34)
15. Ni nani aliyekuwa mkuu wa jeshi la Absalomu, wakati Absalomu alipoasi dhidi ya Daudi, kisha akawa mkuu wa jeshi la Daudi baada ya Absalomu kuuawa? (2 Samweli 17:25; 19:13)
16. Yoabu alimtuma nani ampelekee Mfalme Daudi habari za kifo cha mwana wake Absalomu? (2 Samweli 18:21, 32)
17. Ni nini kilichomfanya Yakobo akate kauli kwamba mwana wake Yosefu alikuwa ameraruliwa na mnyama mkali? (Mwanzo 37:31-33)
18. Malaika aliyemweleza Maria kwamba alikuwa amechaguliwa kumzaa Yesu, aliitwa nani? (Luka 1:26-31)
Majibu ya Maswali
1. Ili ‘watangaze kotekote sifa bora’ za Mungu
2. Kubadili maji yawe divai; Kana
3. Ubavu kutoka kwa Adamu
4. Eli
5. Kori
6. “Ishara za nyakati”
7. Gogu na “umati” wake
8. Kwa sababu ‘mioyo yao ilikuwa mbali naye’
9. Hamu
10. Dani
11. Mtande
12. Tauni
13. Kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Mambo ya Nyakati, Ezra
14. Kilikia
15. Amasa
16. Mkushi asiyetajwa kwa jina
17. Alionyeshwa vazi refu la Yosefu ambalo ndugu zake walikuwa wamelichovya-chovya katika damu ya mbuzi
18. Gabrieli