Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 19. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakivuta makasia kuelekea jiji gani walipomwona Yesu akitembea juu ya bahari? (Marko 6:45-49)

2. Yesu alimpa Simoni mwana wa Yohana jina gani? (Yohana 1:42)

3. Mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati ya ndugu zake anapaswa kuwa nani wao? (Marko 10:44)

4. Yehova alimwagiza Abramu aondoke jiji gani la Wakaldayo? (Mwanzo 11:31; 12:1)

5. Kwa nini Sheria ya Mungu kwa Waisraeli ilishutumu kutafuta ishara za bahati? (Kumbukumbu la Torati 18:10-13)

6. Yesu alisema Wakristo ambao wangewaalika maskini, viwete, vilema, na vipofu kwenye karamu zao wangepata baraka gani? (Luka 14:13, 14)

7. Mtu anapokufa, ni nini hufa pamoja naye? (Mhubiri 9:6)

8. Njia ya Yehova ya kuhesabu wakati inatofautianaje na yetu? (2 Petro 3:8)

9. Wakristo wanaweza kutazamia kupata nini kwa kuzoeza nguvu zao za ufahamu? (Waebrania 5:14)

10. Ni nini kilichofanya Balaamu ampige punda-jike wake? (Hesabu 22:22-25)

11. Ni vazi gani lililofanana na aproni ambalo kuhani mkuu alivaa juu ya koti lake la buluu lisilo na mikono? (Kutoka 28:4, 31)

12. Ni jiji gani lililokuwa la pili kutekwa na Waisraeli walipovamia Kanaani? (Yoshua 8:18, 19)

13. Yesu alisema kwamba kati ya wajane wote waliokuwako wakati huo, Eliya alitumwa kwa mjane yupi tu? (Luka 4:26)

14. Yesu alifundisha kanuni gani kuhusu jinsi ya kushughulika na wale wanaotuchukia? (Mathayo 5:44)

15. Mama ya Sulemani alimfumia nini siku yake ya arusi? (Wimbo wa Sulemani 3:11)

16. Kulingana na maneno ya Sulemani, kwa nini nyakati nyingine wenye mbio hawashindi katika mbio? (Mhubiri 9:11)

17. Wana wawili wa Yosefu ambao walitokeza makabila mawili ya Israeli waliitwaje? (Mwanzo 41:50-52)

18. Yakobo alimwambia Farao kwamba alikuwa amekaa katika nchi ya kigeni kwa miaka mingapi? (Mwanzo 47:7-9)

19. Yesu alikula mlo gani pamoja na wanafunzi wake jioni iliyotangulia kufa kwake? (Luka 22:20)

20. Yule mtu aliyepooza ambaye aliponywa na Petro aliyekuwa amelala juu ya kitanda chake kwa miaka minane aliitwaje? (Matendo 9:33, 34)

21. Ni nani aliyeitwa “mama ya kila mtu anayeishi”? (Mwanzo 3:20)

Majibu ya Maswali

1. Bethsaida

2. Kefa

3. Mtumwa wao

4. Uru

5. Ni aina ya uaguzi unaomchukiza Yehova

6. Wangepata furaha na kuthawabishwa na Mungu, kwa kuwa hawatarajii kurudishiwa chochote

7. Upendo wake, chuki yake, na wivu wake

8. Kwa Yehova miaka elfu ni kama siku moja

9. Ukomavu, kuwa na uwezo wa kutofautisha yaliyo sawa na yaliyo makosa

10. Punda huyo alijaribu kugeuka aende shambani alipoona malaika wa Yehova amefunga njia

11. Efodi

12. Ai

13. Mjane wa “Sarefathi katika nchi ya Sidoni”

14. ‘Wapendeni adui zenu’

15. Shada

16. Kwa sababu ya “wakati na tukio lisilotazamiwa”

17. Manase na Efraimu

18. 130

19. Mlo wa jioni

20. Ainea

21. Hawa