Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kalenda Yenye Kustaajabisha ya Wamaya

Kalenda Yenye Kustaajabisha ya Wamaya

Kalenda Yenye Kustaajabisha ya Wamaya

Na mwandishi wa Amkeni! nchini Mexico

KUREKODI wakati kulikuwa jambo muhimu kwa Wamaya * walioishi nyakati za kale. Imani yao kwamba mambo fulani yangejirudia katika mizunguko fulani ilionekana katika kalenda zao.

Kalenda fulani ambayo wenye mamlaka wanaiita tzolkin (hesabu ya siku) ilikuwa na siku 260 zilizogawanywa katika vipindi 13. Kila kipindi kilikuwa na siku 20, kila siku ikiwa na jina lake la pekee. Kalenda ya tzolkin ilikuwa msingi wa sherehe za Wamaya nayo ilitumiwa pia katika uaguzi.

Wakati huohuo, kalenda ya kiserikali au haab, ilikuwa ikitumika. Hii ilikuwa kalenda iliyotegemea jua yenye siku 365. Ilikuwa na miezi 19, miezi 18 kati ya hiyo ikiwa na siku 20; na mwezi mmoja ulikuwa na siku tano tu, hiyo ikiwa jumla ya siku 365. Utaratibu wa kilimo na maisha ya kila siku ulitegemea kalenda hii ya jua. Wamaya werevu waliunganisha kalenda zote mbili kuwa kile ambacho wachunguzi wanakiita Kalenda ya Duara, na hivyo kutia ndani tarehe kutokana na matukio yote yaliyokuwa katika kalenda hizo mbili. Ilichukua siku 52 ili mzunguko huo wa siku ujirudie. *

Hakuna kitu cha kale kilichopatikana kinachoonyesha kalenda yote ya Wamaya. Wasomi wamefahamu kuhusu kalenda hizo kwa kusoma kwa makini vitabu vya Wamaya ambavyo vimesalia na kwa kuchunguza ishara zilizochongwa katika mawe na sanamu.

Baada ya kuchunguzwa kwa karne nyingi, kalenda ya Wamaya bado inawavutia wataalamu. Ilikuwa na habari ya hali ya juu sana kama vile marekebisho sahihi kabisa yaliyofanywa kuhusu urefu wa mwaka wa jua na rekodi sahihi za mzunguko kuhusu mzunguko wa mwezi na sayari nyingine. Kwa kweli, mambo yote hayo yalihesabiwa kwa ustadi sana na Wamaya wa kale, ambao walirekodi kwa usahihi jinsi wakati ulivyosonga.

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 3 Ona makala “Wamaya Walivyokuwa na Walivyo Leo” katika gazeti la Amkeni! la Septemba 8, 2001.

^ fu. 5 Kwa kuongezea, Wamaya walitumia kalenda iliyoitwa Long Count, iliyokuwa rekodi ya mfululizo wa siku kuanzia siku fulani ya kale ya msingi.

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Tzolkin Haab

6 Caban 5 Pop

Tarehe iliyotiwa alama katika stela iliyo juu ni 6 Caban 5 Pop nayo inalingana na Februari 6, 752 W.K.

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

0 1 5

Wamaya waliunganisha ishara tatu zilizo juu ili kuwakilisha kila nambari. Kwa hiyo,

0 1 2 3 4

5 6 7 8 9

10 11 12 13 14

15 16 17 18 19

Badala ya siku 7, kalenda ya tzolkin ilikuwa na siku 20 zilizokuwa na majina. Baadhi ya ishara hizo zimeonyeshwa hapa chini

Baadhi ya ishara zilizo katika miezi 19 ya kalenda ya haab

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Top right and inset: HIP/Art Resource, NY; glyphs: An Introduction to the Study of the Maya Hieroglyphs/Sylvanus Griswold Morlay/Dover Publications