Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 13. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Katika siku za Sulemani, ni kundi gani la meli lililobeba fedha, pembe za tembo, sokwe, na tausi hadi Israeli? (1 Wafalme 10:22)
2. Alipokaribia kufa, Paulo alionyeshaje kwamba alijua kuwa alikuwa amevumilia? (2 Timotheo 4:7)
3. Ni ndoto gani ya Farao ambayo Yosefu alifasiri kumaanisha kwamba miaka saba ya njaa kubwa ilikuwa inakaribia? (Mwanzo 41:17-24)
4. Ni wanawake gani wawili waliomfundisha Timotheo kwa kutumia Maandiko? (2 Timotheo 1:5)
5. Absalomu alikufa kwa njia gani isiyo ya kawaida, naye alizikwaje? (2 Samweli 18:9, 14-17)
6. Mshahara wa dhambi ni nini? (Waroma 6:23)
7. Yesu alitumia njia gani ya kutilia chumvi ili kuonyesha jinsi ambavyo ingekuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu? (Mathayo 19:24)
8. Ni ofisa gani Mroma wa Yudea aliyemwacha Paulo akiwa amefungwa kwa sababu ya kutaka kupata kibali cha Wayahudi? (Matendo 24:27)
9. Yesu anatajwa kuwa atafanya kazi gani ya kutengeneza divai ambayo inafananisha kuuawa kwa maadui wa Mungu? (Ufunuo 19:15)
10. Hapo mwanzo, zile Amri Kumi ziliandikwaje, nazo ziliandikwa juu ya nini? (Kutoka 31:18)
11. Mtume Paulo alitamani wanawake Wakristo wajipambe jinsi gani? (1 Timotheo 2:9)
12. Ili kuonyesha ukuu wa Yehova, Isaya alisema kwamba Yehova anaweza kupima “maji” katika nini? (Isaya 40:12)
13. Makao ya Adamu na Hawa yaliitwaje? (Mwanzo 2:15)
14. Yakobo alishutumu tendo la jeuri la wana wake gani wawili? (Mwanzo 49:5-7)
15. Ile mito minne iliyotokana na mto uliotoka Edeni iliitwaje? (Mwanzo 2:11-14)
16. Wakristo walio na sifa za kustahili za kiroho wanapaswa kufanya nini mwabudu mwenzao anapokosea kabla ya kujua kosa lake? (Wagalatia 6:1)
Majibu ya Maswali ukurasa wa 13
1. Meli za Tarshishi
2. Alisema: “Nimepigana pigano zuri, nimekimbia mwendo mpaka mwisho, nimeishika imani”
3. Ng’ombe saba waliokonda waliwala ng’ombe saba wanono, na masuke saba ya nafaka yaliyokauka yakala masuke saba ya nafaka yaliyonona
4. Mama yake, Eunike, na nyanya yake Loisi
5. Yoabu na watumishi wake walimwua Absalomu kichwa chake kilipokuwa kimekwama katika mti, na baada ya hapo mwili wake ulitupwa ndani ya shimo kubwa na fungu kubwa la mawe likarundikwa juu yake
6. Kifo
7. Alisema: “Ni rahisi zaidi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”
8. Feliksi
9. Kukanyaga shinikizo la divai
10. “Kidole cha Mungu” kiliziandika juu ya mabamba mawili ya mawe
11. “Kwa mavazi yenye mpangilio mzuri, pamoja na kiasi na utimamu wa akili, si kwa mitindo ya kusuka nywele na dhahabu au lulu au mavazi yaliyo ghali sana”
12. “Katika mkono wake”
13. Bustani ya Edeni
14. Simeoni na Lawi
15. Pishoni, Gihoni, Hidekeli, na Efrati
16. ‘Kujaribu kumrekebisha upya mtu huyo katika roho ya upole