Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Maoni Yanayobadilika-Badilika Kuhusu Rangi ya Ngozi

Maoni Yanayobadilika-Badilika Kuhusu Rangi ya Ngozi

Maoni Yanayobadilika-Badilika Kuhusu Rangi ya Ngozi

KULINGANA na maoni yako, utamfafanuaje mtu mwenye afya nzuri? Je, ni mtu mwenye ngozi laini, iliyogeuka rangi kwa sababu ya kuunguzwa na jua? Watu wengi huko Ulaya na Amerika Kaskazini wana maoni hayo. Lakini haijawa hivyo sikuzote. Miaka mingi iliyopita, wanawake huko Ulaya walivaa kofia pana na kubeba miavuli ili kujikinga na jua. Watu waliokuwa na ngozi nyeupe sana walionwa kuwa matajiri. Watu wenye ngozi iliyogeuka rangi kwa sababu ya kuunguzwa na jua walionwa kuwa watu ambao hufanya kazi ngumu.

Katika nyakati za mapema zaidi, vipodozi ambavyo leo huonwa kuwa vyenye sumu, vilitumiwa kufanya ngozi iwe nyeupe. Kwa mfano, mapema kama mwaka wa 400 K.W.K., Wagiriki walifanya ngozi zao ziwe nyeupe kwa kutumia poda ya uso yenye kaboneti ya risasi. Poppaea Sabina, mke wa Maliki Nero wa Roma, alitumia poda hiyo yenye sumu kufanya uso wake uwe mweupe. Katika karne ya 16, wanawake fulani wa Italia walitumia aseniki kufanya nyuso zao ziwe nyeupe na zing’ae. Lakini tangu mbunifu wa mitindo ya mavazi Mfaransa, Coco Chanel alipofanya mwili uliogeuka rangi kwa sababu ya kuunguzwa na jua uonwe kuwa maarufu mapema katika miaka ya 1920, jambo hilo limependwa na watu wengi. Watu hujianika juani kwa saa nyingi.

Hata hivyo, si watu wote wanaopenda kukaa nje hupenda ngozi yao iunguzwe na jua na kuwa nyeusi. Si kawaida yao kujianika juani. Wao hufurahia kuota jua na kupunga upepo mwanana kuliko ngozi yao kugeuka rangi kwa sababu ya kuunguzwa na miale ya jua. Kwa nini ngozi yao inahitaji kukingwa na jua?

[Picha katika ukurasa wa 3]

Watu wakiwa ufuoni mapema katika karne ya 20

[Hisani]

Brown Brothers