Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 19. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Ingawa Yehova hakutaja kiasi hususa, alitaka taifa la Israeli limpe kilicho bora zaidi kati ya nini? (Kutoka 23:19)
2. Kwa kuwa watu wa Mungu wanafurahia ufanisi na wanaonekana kuwa bila usalama, ni nani anayevutwa awashambulie? (Ezekieli 38:10-12, 14-16)
3. Akifikiria Paulo atamhonga, ni ofisa yupi aliyemfunga mtume huyo kwa miaka miwili huko Kaisaria? (Matendo 24:18-27)
4. Watu wenye ukoma katika Israeli walipaswa kupaaza sauti na kusema nini ili kuwaonya wengine wasiwakaribie na kutiwa unajisi? (Mambo ya Walawi 13:45)
5. Yakobo alitia alama gani kwenye kaburi la Raheli? (Mwanzo 35:20)
6. Kwa nini Yehova aliwapeleka Waisraeli uhamishoni mara kadhaa? (2 Wafalme 18:11, 12)
7. Badala ya kuwa uthibitisho wa hekima inayotoka juu, Yakobo alisema wivu, ugomvi, na kusema uwongo juu ya ile kweli ni sifa za aina gani? (Yakobo 3:15)
8. Ni mti gani ambao Mfalme Sulemani alimwomba Mfalme Hiramu kwa ajili ya ujenzi wa hekalu na kutengeneza vinubi na vinanda? (1 Wafalme 10:11, 12)
9. Yehova alimwagiza Eliya awatie mafuta watu gani watatu? (1 Wafalme 19:15, 16)
10. Ni nani aliyekuwa mkuu wa makuhani “kwa ajili ya kila jambo la Yehova” wakati wa utawala wa Yehoshafati? (2 Mambo ya Nyakati 19:11)
11. Paulo alimshauri Timotheo ajizoeze akiwa na shabaha gani? (1 Timotheo 4:7)
12. Nebukadneza alimshinda Farao yupi wa Misri huko Karkemishi wakati wa utawala wa Mfalme Yehoyakimu wa Yuda? (Yeremia 46:2)
13. Kwa sababu ya busara ya Abigaili, ni jambo gani baya ambalo Daudi aliepuka? (1 Samweli 25:31)
14. Ni maneno gani tofauti ambayo Biblia hutumia inapotaja ndege? (Mwanzo 1:26)
15. Kwa nini kitabu cha Methali kinashauri mtu asitembelee nyumba za wengine mara nyingi kupita kiasi? (Methali 25:17)
16. Kama ilivyotajwa na Petro, ni muhimu kuzuia kiungo gani cha mwili ili kupata kibali cha Yehova? (1 Petro 3:10-12)
17. Ni mnyama gani aliyetolewa kama dhabihu ili kuweka rasmi ukuhani wa Haruni? (Mambo ya Walawi 8:22-28)
18. Kwa nini Mungu aliwakataza Waisraeli wasitie miili yao alama ya chanjo? (Mambo ya Walawi 19:28)
19. Yakobo alipaitaje mahali ambapo yeye na Labani walifanya agano la amani? (Mwanzo 31:43-53)
20. Muujiza wa kwanza wa Yesu ulikuwa upi? (Yohana 2:7-11)
Majibu ya Maswali
1. Matunda ya kwanza yaliyoiva ya udongo
2. Gogu
3. Feliksi, mtawala wa Yudea
4. “Si safi, si safi!”
5. Alisimamisha nguzo juu yake
6. Hawakuwa waaminifu kwa agano walilofanya naye
7. “Ya kidunia, ya kinyama, ya roho waovu”
8. Msandali
9. Hazaeli kuwa mfalme wa Siria, Yehu kuwa mfalme juu ya Israeli, na Elisha kuwa nabii mahali pake
10. Amaria
11. Kusitawisha “ujitoaji- kimungu”
12. Neko
13. Kuwa na hatia ya damu
14. “Viumbe vinavyoruka”
15. Ili wasikuchoke na kuanza kukudharau
16. Ulimi
17. Kondoo-dume
18. Ili kuwatofautisha na mataifa mengine na kukazia heshima ambayo mwili wa mwanadamu unastahili ukiwa uumbaji wa Mungu, yaani, kutumiwa kumheshimu
19. Galeedi (baadaye pakaitwa Gileadi)
20. Kugeuza maji kuwa divai