Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoa Ushahidi Mzuri Shuleni

Kutoa Ushahidi Mzuri Shuleni

Kutoa Ushahidi Mzuri Shuleni

Na mwandishi wa Amkeni! nchini Mexico

DANIEL, kijana mwenye umri wa miaka 17, alipoanza mwaka mpya wa shule, aliazimia kuwajulisha wanadarasa wenzake wapya kwamba yeye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Alipata fursa hiyo wakati mwalimu wake wa somo la Kiingereza alipowauliza wanafunzi wahoji mgeni ambaye lugha yake ya asili ni Kiingereza. Mgawo huo ulitia ndani kusafiri hadi sehemu zinazotembelewa mara nyingi na watalii huko Mexico City, kuwahoji, na kupeleka darasani mahojiano hayo yaliyorekodiwa.

Daniel aliamua kumhoji mmishonari anayezungumza Kiingereza ambaye alifanya kazi kwenye makao makuu ya Mashahidi wa Yehova huko Mexico na, wakati huohuo, kutayarisha video katika Kiingereza inayoonyesha sehemu zote za Betheli ambazo hutembelewa na wageni. Isitoshe, alipanga kuonyesha broshua za lugha mbalimbali za kienyeji zinazochapishwa Mexico na pia gazeti la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika lugha nyingine. Kisha Daniel akamwomba mwalimu wake wa Kiingereza ruhusa ya kuonyesha darasa video hiyo.

Wanafunzi wenzake na mwalimu walishangazwa na kazi inayofanywa na Mashahidi wa Yehova nchini Mexico. Wasikilizaji wa Daniel walivutiwa hasa na jitihada za Mashahidi za kuwafikia wenyeji wa Mexico.

Baada ya kuwaonyesha video hiyo kwa dakika 25, na kupata maksi za juu zaidi, Daniel aliwapa wote nakala za Mnara wa Mlinzi na Amkeni! na vilevile kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi. Wengi walikubali vichapo hivyo, na hilo limefanya watake kuzungumzia Biblia zaidi. Daniel anasema: “Ninamshukuru Yehova kwamba nililetea jina lake sifa kupitia mgawo rahisi wa shule.”