Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Madaktari Hivi karibuni nilisoma makala zenye kichwa “Kuwaelewa Madaktari.” (Januari 22, 2005) Asanteni kwa kueleza waziwazi hisia ambazo madaktari hukabili. Mimi ni muuguzi, nami nimejionea jinsi ambavyo wahudumu wa afya na wagonjwa hukosa kuelewana. Ninatumaini kwamba makala hizo zitawasaidia wengi kuwaelewa wahudumu wa afya vizuri zaidi na kuthamini kazi yao.

L. K., Urusi

Daktari mmoja alinieleza kwamba alisoma gazeti hilo kwa makini. Alisema kwamba lilifanyiwa utafiti vizuri na kwamba anakubaliana kabisa na makala hizo. Asanteni kwa makala hizo nzuri.

H. Z., Ujerumani

Nilipokuwa hospitalini nilikuwa nikijifikiria tu. Lakini gazeti hilo lilinisaidia kuelewa mfadhaiko ambao madaktari hukabili. Kuanzia sasa nitakapokuwa nikitibiwa, sitamweleza maoni yangu kuhusu ugonjwa wangu, bali nitafuata shauri katika sanduku “Kushirikiana na Daktari.” Ningependa kuwa mgonjwa anayejali zaidi.

J. M., Japani

Mimi ni mzee Mkristo na vilevile daktari. Mimi huathiriwa hasa na uchovu unaotokana na kuwahurumia wagonjwa wengi sana ninaowapima kila siku. Kwa kuwa mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova nimeweza kushughulikia kazi yangu kwa usawaziko. Mimi hujaribu kufanya kazi yangu kwa bidii ili nipate wakati wa kuwa pamoja na mke na watoto wangu na wa kushughulikia utendaji mbalimbali wa Kikristo. Gazeti la Amkeni! hunisaidia kuwa na usawaziko na kutokengeushwa kutoka kwa mambo muhimu kikweli.

P. R., Marekani

Sikubaliani na wazo la kwamba “mawakili fulani huwasilisha mashtaka madogo-madogo ili wajitajirishe.” Kwa kawaida mawakili hawalipwi chochote bila uamuzi wa korti au makubaliano kati ya wahusika. Ili kushinda kesi lazima wathibitishe kwamba mgonjwa hakutunzwa kwa njia inayofaa. Kwa kuwa nimekuwa wakili kwa zaidi ya miaka 30, ninaweza kukuambia kwamba nimekataa kesi nyingi sana kuliko zile nilizokubali.

J. M., Marekani

“Amkeni!” lajibu: Kwa kusema “mawakili fulani huwasilisha mashtaka madogo-madogo ili wajitajirishe,” hatukuwa tukizungumzia jinsi tatizo hilo lilivyoenea. Tulikuwa tukisema kwamba madaktari huhangaishwa mara nyingi na mashtaka kuwa hawakuwatunza wagonjwa kwa njia inayofaa. Bila shaka, wagonjwa hutoa mashtaka yasiyo na msingi. Lakini, bado maelezo ya msomaji huyu si mabaya. Mfumo wa sheria una mipaka ambayo inaweza kuzuia mtu asizushe mashtaka yasiyo na msingi.

Vijana Huuliza Nina umri wa miaka 11. Nilifurahia sana makala ya “Vijana Huuliza . . . Nifanyeje Mtu Akinieleza Matatizo Yake?” (Januari 22, 2005) Msichana mmoja shuleni alinieleza kuhusu maisha yake yenye kuhuzunisha. Kuongezea matatizo yake, babu yake alikufa juma lililopita. Nilipata mambo mengi katika makala hiyo ambayo nitatumia kumfariji. Mimi hufarijika sana kujua jinsi Yehova anavyoelewa mambo yanayowapata vijana.

A. H., Marekani

Nina umri wa miaka 14, na vijana wengi wa umri wangu huniomba mashauri. Mara kwa mara kuna matatizo fulani ambayo siwezi kuyashughulikia. Mimi huwaeleza kwa fadhili sababu inayofanya nisiyashughulikie, na nyakati nyingine mimi huwaeleza habari kutoka katika Biblia. Sasa vijana hao huniuliza maswali kuhusu dini yangu. Jambo hilo limenichochea kuzungumzia habari hiyo katika hotuba ambayo nimepewa shuleni yenye kichwa, “Kwa Kweli Mashahidi wa Yehova Ni Nani, Nao Wanaamini Nini?”

B. D., Kanada