Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ulimwengu Uliogawanywa na Utajiri

Ulimwengu Uliogawanywa na Utajiri

Ulimwengu Uliogawanywa na Utajiri

KATIKA sehemu ya pili ya karne ya 20, ulimwengu ulikumbwa na Vita Baridi na kugawanywa kisiasa katika sehemu tatu. Mataifa ya Kikomunisti yakiongozwa hasa na Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Sovieti, na mataifa yasiyo ya Kikomunisti yakiongozwa na Marekani, yalikabiliana kutoka pande mbili za Pazia la Chuma. Mataifa ambayo hayakuunga mkono upande wowote yalifanyiza Ulimwengu wa Tatu.

Hata hivyo, baadaye ilionekana kuwa dharau kuziita nchi hizo “Ulimwengu wa Tatu,” na mataifa hayo yakaanza kuitwa “mataifa ambayo hayajasitawi.” Baada ya muda, usemi huo pia ulionwa kuwa haufai, kwa hiyo wataalamu wa uchumi wakaanza kutumia usemi “nchi zinazositawi.” Hivyo, usemi huo uliacha kukazia tofauti za kisiasa na kuanza kuonyesha tofauti za kiuchumi.

Sasa katika karne ya 21, ulimwengu haujagawanywa katika sehemu tatu za kisiasa zilizotajwa juu. Hata hivyo, bado kuna tofauti za kiuchumi na kiviwanda kati ya nchi zilizositawi na zinazositawi. Watalii kutoka nchi tajiri hukutana na maskini wanaojikakamua kulisha familia zao.

Kwa hiyo, swali hili linafaa: Je, ulimwengu utaendelea kugawanyika kiuchumi, au matajiri na maskini watapata kuwa na hali sawa ya maisha?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

© Qilai Shen/Panos Pictures