Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)

1. Ni nani aliyenunua pango la Makpela kutoka kwa Efroni Mhiti kuwa mahali pa kuzikia, na ni watu wangapi wanaotajwa kuwa walizikwa huko? (Mwanzo 49:30-33; 50:13)

2. Kwa nini wanaume wa Daudi walisisitiza kwamba asiende pamoja nao vitani walipokuwa wakipigana na Wafilisti? (2 Samweli 21:15-17)

3. Ni mmea gani wenye harufu nzuri unaotajwa tu katika Wimbo wa Sulemani? (Wimbo wa Sulemani 1:14; 4:13; 7:11)

4. Gideoni alitumia nini ili awe na uhakika kwamba Yehova angetimiza ahadi yake ya kuokoa Israeli kupitia kwake? (Waamuzi 6:36-40)

5. Beseni kubwa ya shaba iliyotumiwa na makuhani kuogea katika ua wa hekalu la Sulemani iliitwaje? (2 Mambo ya Nyakati 4:6)

6. Jiwe la Waebrania la kupimia lililokuwa zito zaidi na lenye thamani zaidi liliitwaje? (Ezra 8:26)

7. Ni nini kilichotokea mbinguni baada ya Ufalme kuzaliwa? (Ufunuo 12:7)

8. Yesu alisema ingekuwa rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye nini “kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu”? (Mathayo 19:24)

9. Yesu aliwaitaje waandishi na Mafarisayo kwa sababu ya kuwapotosha watu kwa mafundisho ya uwongo? (Mathayo 15:14)

10. Ni mfalme yupi wa Siria aliyewaondoa Wayahudi kutoka kwenye jiji la Yudea la Elathi, na hivyo kumfanya Mfalme Ahazi aogope na kutafuta msaada kutoka kwa Waashuru? (2 Wafalme 16:6, 7)

11. Ni mke gani wa Mfalme Daudi aliyezaa mwana aliyeitwa Ithreamu? (2 Samweli 3:5)

12. Yosefu alipomtuma mtumishi wake awafuate ndugu zake na kurudisha kikombe kilichokuwa kimepotea, kilipatikana wapi? (Mwanzo 44:12)

13. Ni mzao gani wa Kalebu aliyeuawa na Yehova ambaye anatajwa kwa dharau kuwa mkali, mbaya, asiyefaa kitu, na asiye na akili? (1 Samweli 25:3, 17, 25, 36-38)

14. Finehasi alitumia silaha gani ya Waebrania kuwachoma Zimri na Kozbi, na hivyo kukomesha tauni iliyoua Waisraeli 24,000 kwenye Nchi Tambarare za Moabu? (Hesabu 25:6-15)

15. Ni mambo gani manne ambayo Aguru aliona kuwa ya ajabu mno kuyajua? (Methali 30:18, 19)

16. Ni nini kinachotumiwa katika Biblia kuwakilisha mamlaka ya wazazi juu ya watoto wao? (Methali 29:15)

17. Waisraeli walitumia kifaa gani cha kulima kuondoa magugu? (Isaya 7:25)

Majibu ya Maswali

1. Abrahamu. Watu sita: Sara, Abrahamu, Isaka, Rebeka, Yakobo, na Lea

2. Kwa sababu alikuwa amechoka na alikabili hatari ya kupigwa na Ishbi-benobu, jitu la Wafilisti

3. Hina

4. Manyoya ya kondoo

5. “Bahari”

6. Talanta

7. Vita

8. “Tundu la sindano”

9. “Viongozi vipofu”

10. Resini

11. Egla

12. “Katika mfuko wa Benyamini”

13. Nabali

14. Mkuki

15. “Njia ya tai mbinguni, njia ya nyoka juu ya mwamba, njia ya meli katika moyo wa bahari na njia ya mwanamume pamoja na mwanamwali”

16. Fimbo

17. Jembe